-->

MWANAUME! KUWA MAKINI SANA PINDI MWANAMKE ANAPOKWAMBIA MATATIZO YAKO

Image result for mapenzi wakubwa
Mwanamke anapokuambia matatizo yake haimaanishi kwamba analalamika, wala haimaanishi kwamba nilazima umsaidie au akubebeshe hayo matatizo yake. Wakati mwingine anachokitaka ni mtu wa kumsikiliza tu na mtu wa kujua kua anapitia mambo flani na yuko katika kipindi kigumu, mtu wa kumuambia usijali yote haya yatapita mtu wa kumpa moyo.
Mpaka inafikia hatua ya kukuambia matatizo yake inamaanisha kuwa anakuamini na ndiyo maana aliwaacha hata ndugu zake na rafiki zake na kuja kukuambia wewe. Hivyo hembu acha kupaniki. Msikilize hata kama huna uwezo wa kumsaidia inatosha kama utamsikiliza tu. Acha kujifanya uko bize na kumuona kama ni mtu wa kulalamika lalamika, hapana anakuamini ndiyo maana anakuambia.
Kama Dada zako, Kaka zako au rafiki zako wanaweza kumuongelea vibaya mke wako, wakamtukana na kumsengenya mbele yako halafu wewe ukakaa kimya, hata kama kile wanachomzungumzia nichakweli halafu ukajicheklesha chekesha basi jua kuwa sio kwamba wanamdharau au kumchukia mke wako bali jua kuwa wanakudharau na kukuchukulia wewe kama fala flani.
Kazi ya kwanza ya mume ni kumlinda na kumtetea mke wake, hata kama ni yeye ana makosa lakini unapaswa kumtetea na kuwaambia huyu au yule ni mke wangu hamuwezi kumzungumzia hivyo kisha ukaondoka na kuwaacha wakimsengenya. Rudi kwa mke wako mrekebishe kama mwanaume, ana kasoro ongea naye ajirekebishe lakini sio eti mwanaume unachangia kabisa watu wanamsengenya mke wako.
Unashindwa hata na yule mdogo wake wa kike, watu wakikasengenya kale ka bwana kake ambako kanamsumbua kila siku ananuna hata kula hali! Wewe unafurahia kabisa na wakati mwingine unasma ”Kweli mke wangu kazidi! Hata mimi navumilia tu! Sijui hata kwanini nimemuoa!” Jua wanakudharau tena kama ni rafiki zako ukiondoka utawasikia “Hili jamaa fala eeh! Yaani hata halijui kuishi na mwanamke” Ndiyo ukiondoka tnasema hivyo!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU