-->

WANAWAKE WENGI WA SASA WANATAKA KUTAWALA WAUME ZAO

Image may contain: one or more people, people standing and wedding

Kuna kilio cha wanaume nakisikia kikitesa sikio langu, Wanaume wanalia wakisema;
WANAWAKE WA SASA WANATAKA KUTAWALA WAUME ZAO nikaogopa sana kwa kuangalia uhalisia wa NAFASI YA MKE KWENYE MJI nikabaini kwamba ni heshima lakini pia ni ANDIKO LA MUNGU MKE KUWA CHINI YA MUME.
Kilichokuja kunipa tafakari zaidi ni pale nilipogundua kwamba;
WANAWAKE WA SASA WANASIMAMA KAMA MUME kuliko MUME kusimama kama MUME ndani ya nyumba, Na hilo ndilo nikaliona limeangamiza NDOA nyingi, Mume hata awe na uwezo wa kuhudumia familia anakwepa majukumu yake kwa kujua MKE ANAYO NAFASI YA KUSIMAMIA MAJUKUMU YA FAMILI👪
Nikahudhunika sana, Nikamtazama Mwanamke na kumuona ameachiwa majukumu yote ila anakatazwa KUMTAWALA MUME hapo ndipo nikajua kwamba Kwanini WANAWAKE WA SASA WANATAKA KUWATAWALA WAUME ZAO?
Sasa rafiki yangu Mahitaji yote ya familia Mke anasimamia, ada za watoto analipa na Kuna wakati mpaka unampiga kibomu cha mafuta ya gari🚘 KUMBE KOSA NI LA NANI KAMA SIO LAKO?
Kwamba kibesi ni jadi yako ila kusimamia majukumu ya familia unajiwekea upofu kwamba huoni? Wanaume mtawalaumu wanawake kwa ujinga wenu, Wewe mwenyewe ushauvua umwanaume wako ukauacha chumbani kumbe Mkeo afanyeje na anakuhudumia kila kitu? Mwanamke kutaka kukutawala maana yake UTULIZANE SASA mambo ya kibesi nenda kapigie kwenu ila ukifika kwake MPE HESHIMA YAKE MAANA YEYE NDIYE ANAYEKUTUNZIA FAMILIA YAKO.
Yaani hutaki kuambiwa kisa wewe Mwanaume na hujui wajibu wako?
Ndani hutoi MDINYO kutwa unatanga na njia halafu ukirudi Usiku wa manane unataka ukute bakuri la supu? Wanaume tunakosea wenyewe namna ya kuishi na Mwanamke ndo maana napenda kusema MWANAMKE ANAISHI KWA KUFUATA MWANAUME WAKE ATAKAVYO kinyume chake uliishakubali kuhudumiwa unatarajia nini kama sio KUTII?
Hebu simama kama MUME HALISI uone kama Mwanamke atakutawala, Kwanza anaanzaje kukutawala na wewe ndo unamletea vyakula? Anaanzaje kukutawala na wewe ndo unamvisha? Anaanzaje kukutawala na wewe ndiye UNAMPANDA?
Yaani akutawale na anajua Gari umemnunulia wewe kwamba mtaani anatamba kwa nguvu zako?
Sasa wewe kubali kuhudumiwa ili siku ya kuaibika ikifika TUJUE KWAMBA WEWE NI MWANAUME SURUALI na upo kama Mke ndani ya nyumba😅😅😅
Wanaume tambueni NATURE YA MWANAMKE NI KUHUDUMIWA hata akikuzidi uwezo wewe nunua kilicho ndani ya uwezo wako na Mkeo atakipa THAMANI ambayo itakupa nafasi kubwa ndani ya NAFSI YAKE.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU