-->

VYAKULA VINAVYOWEZA KUMPA HESHIMA MWANAUME FARAGHA


No photo description available.
Wanawake wengi walio kweye ndoa wanalalamikia uvivu wa waume zao wanapokutana faragha. Utasikia mwanamke akisema kuwa mumewe ni mchomvu hali inayomfanya wakati mwingine apate mawazo ya kumsaliti. Hiki siyo kitu kizuri na nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba, wanandoa wana jukumu la kushibishana chakula cha usiku bila visingizio. Kama mke au mume ana tatizo ‘sirias’ linalomfanya asiwe fiti, ni vyema jitihada zikafanyika ili kulitatua na kila mmoja afurahie ndoa. Kutokana na hilo, nimejaribu kufanya utafiti na kugundua kuwa, wanaume wengi wanalalamikia suala la kukosa nguvu wawapo faragha. Ndiyo maana nimeamua kuzungumzia vyakula ambavyo wanaume wakila wanajiweka katika mazingira ya kuipata ile heshima wawapo faragha, vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo; 👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼

1.Ndizi mbivu
Ndizi mbivu ni chanzo kizuri cha vitamin B, ambayo inahitajika mwilini kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuondoa msongo wa mawazo. Mbali na kazi hiyo mwilini, pia ina uwezo mkubwa wa kukufanya ujisikie vizuri na kutengeneza hormone zenye nguvu zaidi.

2. Nyama ya ngombe
Nyama ina wingi wa L-Carnitine, ina amino acid ambayo ina uwezo wa kukubusti kwenye tendo la ndoa. Pia ina virutubisho vinavyosaidia kuongeza nguvu mwilini.

3. Boga au mbegu za koli maua
Virutubisho vilivyopo kwenye mbegu za boga au kolimaua husaidia kushtua mwili na kuongeza afya zaidi ya homoni na kuzifanya kuwa na nguvu kwani mbegu hizo husaidia kubusti madini ya chuma. Kama tujuavyo madini ya chuma huhitajika zaidi kwenye mbegu za kiume pia humfanya mtu kuwa na afya zaidi.

4. Cocoa au chocolate
Cocoa au chocolate ni nzuri kuweka kwenye mlo wako kwa maana ya kuulinda moyo ambapo wataalam wanasema kama moyo wako ni imara basi hata zoezi zima la faragha litaenda vizuri. Cocoa ina uwezo wa kupunguza cholesterol pamoja na presha ya damu. Pia cocoa ina uwezo wa kuongeza matamanio kutokana na virutubisho vilivyomo. Yaliyomo kwenye cocoa pia yamo kwenye chocolate nyeusi, hivyo ukikosa cocoa pendelea kunywa chocolate nyeusi.

5. Karanga mbichi, korosho na mrozi
Virutubisho vilivyomo kwenye karanga mbichi, mrozi na korosho vinasaidia sana kwani vina nitric aside ambapo inasaidia mwilini hasa katika kubusti homoni na kuupa mwili nguvu. Hizo ndiyo aina za vyakula ambavyo vinaweza kukupa heshima faragha hivyo ni vyema ukaanza kuvitumia.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU