-->

USIRUHUSU UTANI UKAHARIBU MAHUSIANO YAKO.

Moja kati ya vitu vitakavyokupotezea sifa ya kuwa mke au mume bora na mwenye kujiheshimu ni kuruhusu mtu yeyote kufanya utani oliovuka mipaka katika mwili wako, kukukombatia na kukushika shika katika hali ambayo inaweza kuwa na viashiria vya usiliti ndani yake.
Inawezekana jambo hili linaweza kuwa la kawaida sana kwako, kwakuwa umekuwa ukifanya kwa matani bila kukusudia lolote kutokea ila ukijaribu kufikiria kwa upande wa pili nini kitatokea pindi mumeo au mkeo akishuhudia namna ambavyo unataniana na wafanyakazi wenzako au watu wengine..
Mara nyingi jambo hili limekuwa likiwakumba sana wake au wenza wa watu. Hivi inakuwaje mke wa mtu unakubali kutaniwa kirahisi na wewe unaonekana kufurahia tu? Ni utani gani huo wa kusifiana maumbile au kushikwashikwa kisha unachukulia poa?
Kama ulikuwa hujui, wanaume wengi wanapofanya utani na wake za watu, wanatengeneza mazingira ya kutongoza na wachunguzi wanaeleza kuwa, mke wa mtu anapotongozwa na mtu ambaye wamekuwa wakitaniana sana tena ule utani wa kijinga, ni vigumu kuchomoa yaani hawezi kukataa. Sasa kwa nini uiweke ndoa yako rehani kwa kuweka mbele utani wa kijinga? Kwa nini usiiheshimu ndoa yako kwa kujiweka mbali na wanaume ambao wanaweza kuibomoa ndoa yako?
Wanawake wengine ni wa ajabu sana. Unamkuta anajenga ukaribu na baadhi ya wanaume na kufikia hatua ya kutaniana nao katika mambo ambayo mwishowe huwa kutongozana. Mwanamke aliyeolewa au mwenye mpenzi wake hatakiwi kujenga ukaribu uliovuka mipaka na wanaume wa pembeni. Cha msingi ni kuwaheshimu na kutowachukulia kuwa ni maadui.
Unapopita maskani wamekaa wavulana au unapokuwa ofisini na sehemu nyungine wasalimie kisha chukua hamsini zako, utani wa kijinga epukana nao kwani mwisho watakutongoza na ukionesha kuchukia watadai walikuwa wanakutania kumbe wako ‘sirias’. Jiheshimu.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU