-->

HAWA NDIO MAADUI WATANO WA MWANADAMU.


Mwanadamu au binadamu ana maadui wanaomzuia au kumpinga katika maisha yake hapa duniani. Ili asifike katika malengo yake na asifike mahali mungu alipomwandalia kufika.
ADUI WA KWANZA: MAZINGIRA.
-Mazingira yanaweza kukuzuia usifike katika hatima yako ama usifike kwenye kile kitu alichokuandalia Mungu. Kuna watu wengi wanaangalia mazingira ndiyo maana wameshindwa kufika alipowaandalia Mungu.
YEREMIA 1:6-7.
ADUI WA PILI: MWANADAMU.
-wanadamu wanaweza kukuzuia au kukuinukia kukupinga ili usifike alikokuandalia Mungu. Mwanadamu hukatishwa tamaa na Mwanadamu na Mwanadamu hupigwa na mwanadamu mwenzake.
.Ni wanadamu wachache wanaopenda wewe ufike sehemu aliyokuandalia Mungu. Lakini wote waliokuzunguka awatataka ufike alikokuandalia Mungu .Usizani kundi kubwa La watu lililokuzunguka na kukushangilia ukazani wanapenda ufike alikokuandalia Mungu kufika wengi hawapendi na wako karibu na wewe ili kutafuta anguko lako na kushindwa kwako.
MATHAYO 10:36.
ADUI WA TATU HOFU:
-Hofu ni mlango Mkubwa wa kukufanya ushindwe kufika alikokuandalia Mungu. Hofu huua kila kitu ulichokuwa nacho ndani.Hofu itakuonesha kuwa hauwezi .Ukiwa na hofu utajiona unaudhaifu Mwingi itapelekea kukata tamaa na kujiona hauwezi jambo lolote. Hakuna kitu cha kuogopa Katika maisha Kama Hofu.
Isaya 41:10-11
ADUI WA NNE SHETANI:
-Shetani ni dui mkubwa wa mwanadamu. Adui wa shetani ni mwanadamu na Adui wa mwanadamu ni shetani.
.Shetani ndiyo chanzo cha kila kitu katika Maisha yako kila kibaya kinachokufika .
.Shetani hataki upokee chochote katika Maisha yako hata Kama Mungu amekupa yeye hutaka Kukunyang'anya.
.Shetani hukupinga hukupinga kila Siku na kukuibia kila siku ili usikae na Kitu.
.Shetani ni Mwizi akija katika Maisha mtu huja kuiba na kuaribu, na kuchinja, na kuua chochote kile ulichokuwa nacho katika Maisha yako.
YOHANA 10:10
*.Ukiona unafeli mambo haya yaangalie Sana katika Maisha yako. Huwezi kufaulu bila kuyashinda mambo haya , Huwezi kufika alikokuandalia Mungu pasipo kuvitambua vitu hivi katika maisha yako.
Tambua Mazingira yako yasukushinde usitawaliwe na Mazingira bali wewe yatawale Mazingira, Usitawaliwe na Hofu bali wewe itawale hofu, usitawaliwe na shetani Ila wewe Utawale.
SHARE ujumbe Huu kwa Mwenzako.
AMEN.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU