-->

IFIKE MUDA MJUE KWAMBA KILA JAMBO LINA MUDA WAKE, UKIFIKA LITAPITA TU, HATA KWENYE MAPENZI PIA.

KILA JAMBO NA MAJIRA YAKE... Wala huna sababu ya kujiumiza katika mambo ambayo yana majibu yake kwa moyo, Sio lazima arudi ama akutafute, kilicho cha THAMANI ni yeye kutolala bila kukumbuka yale mazuri ulimtendea, akifikiri japo kwa sekunde moja juu yako na kuyakumbuka yale mlishirikiana INATOSHA SANA KUKUFANYA UENDELEE KUWA WA THAMANI KWAKE! Ni kweli hakuna mkamilifu chini ya JUA lakini unasomeka kwa wema na huruma juu yake na ndo maana KULE ALIKO KUNAMFANYA AJUTIE lakini anateswa na aibu kwa kile alikutendea, Kwa upande wako INATOSHA kujuwa kuwa hukumtendea ubaya wa malipo yale amekulipa, Wala usisumbuke kuuambia umma juu ya wema wako kwake maana umma unajuwa kiasi ulimpenda na kumvumilia kulingana na tabia zake, Usisononeke na kujipa mawazo ambayo yatakukondesha wakati Kuna watu wanalo pendo la dhati wakihangaika wapi walitue... Furaha yake ni kukuona ukikonda na kuharibu mwonekano lakini hebu ondoa mawazo hayo yakutesayo na uinuke ukaangaze maana utaonekana na hapo ndipo atakapojuwa tena THAMANI yako lakini isikubari arudi Kwani atataka kujuwa siri ya FURAHA yako inatokana na nini ili akurubuni uhalibikiwe, Mwenye UPENDO hutazama ASUBUHI na ifikapo MCHANA hufurahia ili kuusogeza USIKU apate kupumzika iweje yeye hakujuwa UMUHIMU wako halafu leo anajifanya anajuwa? Achana nae ANAKUCHELEWESHA KUYAFIKIA MALENGO YAKO.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU