-->

USIRUHUSU MTU AWAYE YEYOTE KUCHEZA NA NAFSI YAKO"

Image may contain: one or more people, text, outdoor and water

Tuliumbwa kwa mfano wa MUNGU! Ndo maana tupo tofauti na viumbe vingine, Lakini kumbuka WANYAMA, NDEGE, SAMAKI nao wana mioyo, figo, maini, bandama na mapafu ambayo nasi bin adam ndo tulivyonavyo, Tofauti kubwa tuliyonayo na viumbe vingine ni kwamba sisi tulipewa UFAHAMU! Na kwa ufahamu huo ndo tumekuwa na UTASHI na hapo ndipo tunaonekana hatuko kama viumbe wengine, Wanyama ama viumbe wengine HAWAUANI AMA KUUMIZANA KWA KUPANGA bali hupambana kulingana na tukio lenyewe maana wao hawana UFAHAMU... Bin adam anaweza kukuumiza, kukuua, kukusengenya, ama kukutendea ubaya wowote kwa sababu moja tu ANAPANGA HAYO KWA UFAHAMU WAKE! Wengi watapanga mabaya juu yako ili kusuuza mioyo yao, lakini wao hawajui kuwa unayo NAFSI inayohitaji FURAHA NA AMANI... Jambo kubwa ambalo litakusaidia wakati wa mapito yako ni hili "JISIMAMIE KI FIKRA NA KI MTAZAMO ILI USIRUHUSU MTU AWAYE YEYOTE KUCHEZA NA NAFSI YAKO"
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU