-->

USIOLEWE AMA KUOA KWA SABABU YA KULIPIZA MAHUSIANO/NDOA UTAKAYO🚦


Image may contain: 2 people, indoor
Kuna watu wanadhani ili kuendana na hali ya AMANI ni pale unapokuwa umevunja uhusiano ama ndoa na kupata mtu mwingine, Kwamba watu wengi kwa sasa anafikiri kuwa na Mtu mwingine tena anayemzidi uliyekuwa nae iwe kwa muonekano ama nafasi hiyo ndiyo suruhu ya tatizo alilolipata HUKO NI KUJITAABISHA TU.
Kumbuka kwamba kulipiza ni DHAMBI lakini pia wakati unalipiza utakuwa UNALAZIMISHA ULIYEMPATA AKUPENDE BADALA YA YEYE MWENYEWE KUKUPENDA kitu ambacho kwako itakuwa FAIDA ya wakati huo na ndiyo HASARA ya baadaye, Huwezi kumlipiza Mtu kwa kupata mwingine kwa sababu MAPENZI ni kitu kinachositawi na kunyauka, Hata mkipendana kwa kiwango gani Kuna KIFO na mmoja akifa mwingine ataomboleza na baadaye atahitaji Mtu mwingine, Sasa unajitaabisha nini kulipiza na kumbe KUACHWA KUPO TU? Tatizo ni njia ipi inatumika kuachana, Unaweza kujidanganya kwamba ULIYEMPATA NI BORA ZAIDI KULIKO ULIYEKUWA NAE lakini kwa hesabu hiyo hiyo jiulize;


 KAMA ANGEKUWA BORA UNGEMPATAJE IKIWA NI MTU MZIMA NA ALIISHAKUWA NA MAHUSIANO YA HAPA NA PALE INA MAANA UBORA WAKE HAUKUTAJWA HUKO ALIKOPITA?"
Mapenzi hayalipizwi Kwani ni TENDO LA UTASHI hivyo huna sababu ya kumlipiza mwenza wako kwa kumuonyesha kwamba alipokuona wa nini Kuna ambaye anakuona wa THAMANI.
Safari ya MAPENZI ni kama safari ya PORINI ni ngumu kuujua USALAMA wako kwa asilimia 100 Lakini ni rahisi kuamini kupitia MATENDO.


Siku zote AWALI ni AWALI tu wala haiwezi kufanana na MWISHO ndo maana katika kuyaenenda MAPENZI yakupasa kujua kwamba KUNA UHALISIA WA BIN ADAM hivyo usijiamini kupita kiasi wala usiamini sana, Kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kuweka BALANCE ndani ya moyo wako na kuepuka MAUMIVU YA MAPENZI ikiwa Muda wake utakwisha, Jifunze kupitia makosa yaliyokufanya ukaumia, Lakini pia nikwambie kwamba USIAMINI SANA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA kuliko kuboresha yaliyopo Kwani hayo tayari unajua madhaifu yake ni rahisi sana KUYAISHI kuliko kama ukitafuta Mengine, Tatizo lililokuumiza haliwezi kupona kwa kupata mwingine kwa sababu hata huyo mwingine ni bin adam aweza kukuumiza vile vile ama zaidi ya vile, Fikiria zaidi wakati unataka kulipiza JE HILO NDILO LITAMFANYA X WAKO KUUMIA? Ni kweli anaweza kuumia JE MAUMIVU HAYO YATADUMU KWAKE? Na je wewe utaona ndo AMANI YAKO KUMTENDEA VILE? Baada ya hayo maswali Jiulize;


 NINI BAADA YA MALIPIZI HAYO😎
Mapenzi hayalipizwi ila yanaachwa kama yalivyo, Kwa sababu uyaonayo leo pengine kesho usiyaone ITAKUFAA NINI KULIPIZA NA MWENZA WAKO AKAENDELEA KUKUPENDA VILE VILE?
Fikiria zaidi kuitafuta AMANI ili uweze kuutuliza MOYO WAKO Mengine uyaache yaendelee kwa sababu ni sehemu ya udhaifu wa bin adam, Usiutaabishe MOYO kumuwazia aliye kuumiza na kumtafutia HUKUMU maana UPENDO HAUDANGANYWI zaidi HASIRA ni TUNDA LA AKILI😅😅😅
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU