-->

Ukitaka kujua MAHUSIANO YAKO YANA NGUVU KIASI GANI UKOSE SMARTPHONE📱


Image may contain: 1 person
Kwa sasa ili mtu akukumbuke ni mpaka uwe na smartphone, Ukiwa WATSAPP ni rahisi kwako kuamsha hisia za mwenza wako pindi unapobadili DP😅😅
Ukiwa instagram ukapost ka picha akiona tu KIMUHE MUHE kinampanda na utaona ka msg inboboooo kama sio kukupigia simu, Na hapo ndipo unagundua kumbe kwa sasa hatuna UPENDO bali tunaishi kwenye MAHUSIANO yaliyotawaliwa na SMARTPHONE📱
Kwamba kwa sasa ili mtu afurahie MAHUSIANO lazima uwe kwenye utandawazi je hilo ndilo limebeba maana ya UPENDO?
Ni ujinga kuona Mpenzi wako ili akutafute ni mpaka akuone ONLINE nawe bila kujua kwamba wewe level yako WATSAPP masikio yanakusimama kama PANYA🐀 ndo unaanza kuchat.
Ndo maana MAHUSIANO yetu yamekuwa kama BIG G Yaani kupata mpenzi ni rahisi mno na kuachana ni kama kutema mate yakijaa mdomoni 😅😅
Ukikosa MB na MAHABA umeyakosa, Akikosa MB nae hapati MAHABA Yaani smartphone📱 ndo imekuwa sababu ya MAPENZI?
Bahati mbaya ukapoteza ama ukiharibikiwa smartphone📱 ukarudi kwenye TORCH🔦 hapo ndo umeliweka REHANI penzi lako, Kwa sasa mtu anapambana kujiunga INTERNET kuliko hata kifurushi cha kupiga na msg za kawaida, Wengine ndo Ukikosa Smartphone hagusi msg za kawaida, Nawe una Torch 🔦 kwa hakika Kuna haja ya kujua UHUSIANO wako umebebwa na nini? Maana kama ndo umebebwa na Smartphone nawe haupo hewani😭😭😭
Mpaka uje kurudi unakuta TOFAUTI YA HALI YA JUU💔
Kataa Mapenzi ya simu, Akikupenda atatumia simu kujua Uko wapi ili aje kukufikishia ujumbe wa MOYO WAKE kuliko kujifanya anakupenda wakati ni mpaka akuone ONLINE ndipo ajifanye kusema "Hi"
Vinginevyo UNAKULA UPEPO🌊
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU