-->

MALIZA UGOMVI KABLA HUJATAKA KUENDELEA AMA KUTOENDELEA KWENYE UHUSIANO/NDOA ULIYOPO;

Image may contain: cloud, outdoor, nature and text

Usiondoke kwenye ugomvi huku hamjaridhiana vizuri, siku zote kumbuka kwamba kiini cha tatizo hicho ndicho mnatakiwa kukijua na kukimaliza, Ni ujinga KUTAFUTA USHINDI AU KUUMIZA mwingine kisa wewe unaonekana kuwa juu yake kwani KUTATUA TATIZO kunakufanya uwe na AMANI moyoni, lakini pia kumfanya mwenzio kuwa na AMANI.
Usifikirie KUKIMBIA TATIZO bali unaweza kulitatua ama kwa kulimaliza liishe ili KUENDELEA mkiwa na AMANI au KUTOENDELEA lakini kila mmoja akawa na AMANI ili hata mkikutana mnaweza kusalimiana, Kuondoka mahala huku umeacha ugomvi baridi ujue hata uende wapi UTAISHI BILA AMANI kwa sababu mahusiano au ndoa yoyote ile hata kama hamkupendana Kuna kitu kinaitwa MAZOEA hicho ndicho ambacho kitakugharimu pindi utakapo kuwa umeamua kumuacha mwenza wako mkiwa hamjakubaliana kuachana.
Ya nini kujitesa na wakati MAISHA YENYEWE MAFUPI?
Kujipa stress kufikiria uliyemuumiza anawaza nini INAHUSU?
Kupendwa na Kutopendwa yote yapo kwenye uwezo wa UTASHI WA MTU hivyo kuliko kumbeba moyoni Mtu asokupenda kisa unataka kumlipiza bora UKAMUACHA NA HAMSINI ZAKE ili uendako ukawa huru moyoni kwanza ni rahisi hata kumpa nafasi mwingine.
Maana wewe ndiye utakaye taabika na mwisho wa yote MWENZIO anaendelea na maisha yake na pengine wala hakufikirii wala kukumbuka kama nawe uliwahi kuwa nae😅😅😅
Mwache aende akiwa HURU nawe akuache na UHURU wako pengine atakuja mtu sahihi ambaye atakusahaulisha UNYONGE WAKO Kwani kung'ang'ania MTU AENDELEE KUWEPO wakati moyoni amechoka kuwa nawe ni HATARI lakini pia ni HASARA KWAKO.
Kawaida ya kuachwa ni MAUMIVU lakini kwa kitambo kidogo na huku ukiwa umeijua THAMANI yako utapona na kuelekea mbele, Pengine ukasema jana ilikuwa mbaya kuliko leo BE STRONG💪ENOUGH.
#Elista_Kasema_ila_Sio_sheria🔨
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU