Uzuri wako wa nje usikufanye uwe na fikra za kwamba anayetakiwa kuwa na wewe ni mwanaume mwenye kipato kizuri na mwonekano wa kuvutia kisha ukasahau unahitaji mtu mwenye akili na atakayeheshimu hisia zako.
Kila siku haudumu kwenye mahusiano na hutaki hata kuangalia ni watu wa aina gani unahusiana nao ili uweze kujitathmini na kubadilika. Umekua tu unaangalia wenye vitu na sio utu kisha wakianza kukusaliti unaanza kusema wanaume wote ni sawa.
Usipobadili tabia, chaguo pamoja na mtazamo wako wanaume wote wataendelea kuwa sawa na hutofurahia mahusiano yoyote hapa duniani.