-->

UKIAMBIWA NDOA NI KUVUMILIA JIULIZE HIVI KWANZA..


JE NINI CHA KUVUMILIA NA KWA SABABU GANI??Rafiki yako anapokuambia ndoa ni uvumilivu na anapokuambia hata yeye anavumilia hembu jiulize anavumilia nini na kwa sababu gani?
Kuna mtu anavumilia kwasababu hana kazi na siku akipata basi anaondoka.
Kuna mtu anavumilia kwakua kazi anayoifanya haimpi aina ya maisha ambayo anayataka hivyo analazimika kuvumilia ili aendelee kuishi vizuri.
Kuna mtu anavumilia kwakua anajua sababu ya kumpata huyo mwanaume/mwanamke labda aliloga sana na sasa anachokipata ni matunda yake.
Lakini kuna mtu anavumilia kwakua kama ni magonjwa kashaambukizwa hivyo anaona kua hata akiondoka hakuna kipya huko nnje,
Lakini kuna mtu anavumilia kwakua moyo wake ushakufa ganzi hahisi tena maumivu ashajikatia tamaa na maisha yake.
Kwamaana hiyo, usidanganywe na tabasamu lake la nnje pale anapokuambia Vumilia, bali angalia anavumilia kwa sababu gani na wewe jiulize unataka uvumilie kwa sababu gani?
Je, ni kwamba umeizoea hiyo hali na hutaki tena mabadiliko?
Je, kuna matumaini kua kutakua na mabadiliko mbeleni?
Je, huna pakwenda na kila mtu anakuona mzigo?
Je, umeshachoka maisha na huna mpango wa furaha tena?
Je, kashakuambukiza kila ugonjwa na hakuna jipya la kukupa?
Ndiyo acha tu kuvumilia kwakua kila mtu anavumilia,
Wewe si kila mtu,
Wewe si wao,
Maumivu yako si yao
Na
Wala maumivu yao si yako.
Nilazima ujifunze kufanya mambo kwaajili yako na si kufanya mambo kwakua kila mtu anafanya.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU