Ninaandika haya ili uelewe kwamba ni vizuri kuwatambua wenza wetu na mchango wao licha ya mapungufu yao.
Nina umri wa miaka 32. Mimi na mume wangu tulikaa kwenye uchumba kwa miaka 6. Tulikuwa marafiki sana.
Nilimsubiri mpaka alipomaliza masomo yake ya chuo na kuanza kazi.
Familia yangu na yake zilikutana, tukaoana na kupata mtoto ambaye kwa sasa ana miaka 7.
Wakati mwingine mume wangu alikuwa mwenye hasira za karibu lakini matatizo yetu yalianza pale nilipotaka kumfanya ajihisi kuwa hawezi kunidhibiti.
Kila wakati tulipojibizana, nilifunga mabegi yangu kwenda kwetu na kuieleza familia yangu.
Dada zangu walikuwa wakimpigia simu mume wangu na kumfokea.
Akinikatalia jambo au kunidhibiti nilikuwa nikimtishia kwamba kama anataka anipe talaka yangu.
Sikuwa nataka talaka kweli, bali nilikuwa na kiburi na sikutaka nionekane kuwa ni mwanamke rahisi na dhaifu mbele yake.
Siku moja nilimsukuma sana kiasi kwamba alishindwa kuvumilia na kwa mara ya kwanza akanipiga na kunifungia nje.
Nilienda kwa wazazi wangu. Ndugu zangu walimripoti polisi, kila mara nilijifanya kana kwamba nilikuwa nanyanyaswa.
Lakini kwa kweli, mimi nilikuwa nikimnyanyasa mume wangu kiroho na kihisia.
Alikamatwa na kufungwa. Familia yake iliniomba nifute kesi. Nilihisi kwamba nilichofanya hakikuwa sahihi.
Mume wangu hakuwa mtu mgomvi, alifanya aliyoyafanya kwa sababu nilimsukumia ukutani. Alipiga magoti na kuomba msamaha. Nilimsamehe, nikafuta kesi na tukasuluhishwa.
Baada ya miezi 3, nilifungasha mabegi yangu tena baada ya kutokea tatizo kidogo, nikaondoka akabaki peke yake.
Siku mbili baadaye nilipokea simu kwamba alikuwa hospitali.
Ndugu zangu waliniambia kwamba sipaswi kwenda kumjulia hali kwa sababu ingeonekana kana kwamba najikomba kwake, na hata dada zangu waliamini kuwa hakuwa mgonjwa bali alikuwa akiongopa.
Muda wote huo, watu walinisikitikia kana kwamba mimi ndiye niliyekuwa nikinyanyaswa.
Alikaa wiki moja hospitalini, alipotoka nilipokea wito wa talaka.
Nilitaka kuikataa talaka, lakini kwa kuwa nilijihisi kiburi, nilitaka yeye ndio abadilishe nia na kuniomba tuendelee kuwa pamoja.
Nilimpigia na kumwambia anipe talaka yangu kwa sababu niliishi kana kwamba niko motoni.
Nilipoenda mahakamani, nilitaka kumfanya ajutie, niliiambia mahakama kuwa nataka tugawane mali zake.
Kwa mshangao aliiambia wazi mahakama kuwa mali ambazo mimi na yeye tulichuma pamoja nikabidhiwe zote, yeye anachotaka ni kuachana na mimi.
Tuliachana rasmi Julai 2009.
Kwa sasa mtalaka wangu ana mke mwingine, wakati mimi nikiwa hapa nimetelekezwa!
Mwanangu pia anakosa upendo na usuhuba wa baba yake.
Ndugu zangu wananisengenya na kunisema vibaya.
Maisha yangu yanategemea kile ambacho mwanangu anapewa na baba yake.
Najua niliichezea bure na kuipoteza ndoa yangu.
Niko hapa kuwaambia wanawake kwamba wanapaswa kuwa makini kuhusu ushauri wanaopewa na watu.
_*Usidanganyike, usiruhusu watu wakaingilia ndoa yako.*_
Hata dada zangu wadogo wanaheshimiwa kuliko mimi.
Wale waliokuwa wakinichochea niachike ndio ambao muda wote wananicheka na kunidharau.
Tafadhali dada zangu, shikamana na ndoa yako na uilinde vikali.
Ni rahisi mumeo kukuacha kama unaendelea kumvunjia heshima na kumkosea adabu. Atafanya hivyo bila kujali elimu yako, cheo chako na historia yako.
Niliona vyema niwashirikishe simulizi yangu ili mpate kuziokoa ndoa zenu.
Hakuna faida ya kuwa na kiburi kisichokuwa na manufaa.
*WAKATI MWINGINE HUWA SIO KOSA LA MWANAUME KABISA, BALI NI KIBURI CHAKO NA WALE WATU UNAOWARUHUSU KUKUSHAURI, HIVYO TUMIA HEKMA NA BUSARA KATIKA NDOA YAKO*.