Bali kuna mahusiano watu wanaingia ili kutafuta nafuu ya mahangaiko wanayopitia kwa wenza wao, iwe kwa dhiki ama kwa sababu za ki mwili lakini yote ni kuganga MIOYO...
Mwenye kuumizwa ni yule ambaye ameamini kwa uhusiano aliopo, kwa sababu aliyekuja kwa sababu zake atajitahidi kudanganya na kuficha uhalisia wake bila kujua madhara yatakayo mpata ambaye yeye ATAWEKEZA MOYO WAKE AKIAMINI AMEPATA na kumbe ndo kwanza anayo safari ya kutafuta🙆
Mapenzi ni kama UPEPO❄ kuna wakati yanaleta FURAHA kwa hakika nyakati hizo ni FARAJA iletayo AMANI na kunenepesha MOYO 💌
Ila kuna wakati mwingine Mapenzi hayo hayo husababisha SIMANZI😠kwa hakika majira hayo hudhoofisha mwili pamoja na kukosa NURU usoni,
JE TUSIWE KWENYE MAPENZI?
Jibu ni HAPANA🚫
kwani bin adam kamili hayakwepi MAPENZI bali anao wajibu kujua THAMANI YA MAPENZI ili kumpa UPENDO mwenza wake ikiwa kuna UPENDO anaupokea kwake, Mapenzi yakikosa MVUTO YAMEKUFA Kwani kila hatua kwenye mahusiano huleta elimu ya kujenga HAIBA lakini kama kila ukijiuliza MBONA MAHUSIANO YANGU HAYANIPI FURAHA?
Haraka sana tafakari mambo makuu mawili;
▪ NIPO KWENYE PENZI HILI KWA
SABABU ZIPI?
▪ MWENZA WANGU ANAJUA KWAMBA
NAMPENDA?
Maana unaweza kujikuta unapoteza MUDA kwa kungojea muujiza wa utulivu wa penzi lenu wakati mwenzio hana malengo nawe, lakini pia ukaishi na mtu ambaye hahitaji KUPENDWA KWA KIWANGO AMBACHO UNAMPENDA NACHO kumbe mwenzio alikuwa kwenye mtazamo wa REFRESHMENT
Jichunge kuzamisha MOYO wako kwa papara kwa mtu ambaye hasomeki ni mwenye upendo ama ni mpitaji, sababu utulivu Una maswali na majibu sahihi kwa hitaji lako hivyo jipe muda mwingi ukiwa mtulivu ili kubaini ishara za MUONGO NA MNAFIKI.
#Elista_Kasema_ila_Sio_She