-->

NAOMBA USOME KWA MAKINI UTANIELEWA

Unamjua jongoo? Najua jibu lako ni "NDIYO".
Ana miguu mingapi? Najua hujui idadi ila jibu lako ni "MINGI"
Ana macho? Najua jibu lako ni "HAPANA"
Okay..
Unamjua chura? Najua umesema "NDIYO"
Ana miguu mingapi? Najua umesema "MINNE"
Ana macho? Najua umesema "NDIYO TENA MAKUBWA"🐸
Okay kati ya jongoo na chura nani mwenye spidi kubwa? Najua umesema ni "CHURA".
Ndo hivyo. Wingi wa miguu siyo ukubwa wa spidi. Miguu mingi bila macho is a disaster. Ukiwa na miguu mingi unakuwa umenyimwa uwezo wa kutembea unalazimika KUTAMBAA TU yani huna tofauti na ambaye hakupewa miguu kabisa.
Mwenye michache anakuwa amepewa uwezo wa KURUKA na kukwepa hatari kirahisi. Labda awe mjinga asijue siri hiyo.
Usilalamike kuwa na "miguu" michache. Chunguza uwezo wako wa kuruka umefichwa wapi. Hutakaa umwonee wivu "jongoo" hata siku moja. Itafika hatua utamwonea huruma tu. Ajabu ni kuwa usijeshangaa jongoo akamwonea huruma chura kuwa kwa nini anahangaika kurukaruka badala ya "kuslide" tu mdogo mdogo😀
Haya. Si unajua jongoo ukimgusa tu ANAJIKUNYATA. Watu wengi wako hivyo. Hataki shida. Hataki challenge. Akianza biashara challenge kidogo ANAACHA.
Mguse chura uone. Anaweza kuruka mara tatu mfululizo.
Mpige teke jongoo unaweza kuondoa uhai wake dakika hiyo hiyo. Mpige teke chura umemsaidia kufika haraka aendako.
Okay.. tazama hili pia.
Ngozi ya jongoo ni ngumu. Lakini kumbe ni rahisi kuchanika na kuiunga tena inakuwa impossible. Chura je? Ngozi yake iko ELASTIC. Inavutika. Haichaniki labda kwa kisu siyo vitu vidogodogo eti kumpiga teke akaenda akajigonga ukutani. Ataamka na kuendelea na safari ya maisha kama kawaida na utashangaa. Wakati hapo jongoo maisha yangeshaishia hapo. Kuna watu ni jongoo. Akikutana na changamoto ndogo tu kwake inammaliza kabisa. Hana uimara wowote.
Sad. But true.
Be like a frog. #YouCanGetTheGold
Semper Fi,
AGM
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU