-->

UNAYO HIFADHI MOYONI MWAKO YANAWEZA KUKUTIA UNAJISI


Hapa kulikuwa na habari ya kile kimtokacho Mtu au kimwingiacho, Yesu akaweka wazi kitu gani kinaweza kumtia Mtu unajisi
_
Leo nataka kuzungumzia umuhimu wa kuwa na Neno la Mungu moyoni mwako kwasababu, ndani ya moyo wako ndio mambo mabaya yanapotoka Kama Neno lilivyotuambia
_
Ili Roho Mtakatifu aweze kukusaidia ni muhimu wewe kuwa na Neno la Mungu kwa wingi ndani yako ili usitende dhambi Kama livyoandikwa kwenye
Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
_
Kwasababu Neno la Mungu ni Waebrania 4:12-13 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.
_
Kwa hiyo ukiwa na Neno la Mungu kwa wingi ndani yako, uchafu hautakaa
_
Ndio maana tupo hapa kufundishana, kuelemishana na kukumbusha juu ya Neno la Mungu
_
Ukiwa na watu wako unapenda, wajifunze wakaribishe kwenye hii page, kwa maana tupo hapa kwa kazi hiyo tu, kukufundisha ili upate kuijua kweli
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU