-->

NAOMBA UISOME HII KWA MAKINI KABLA HUJALALA.

Mara nyingi Wanawake wamewapa Wanaume malezi ya kuwajali, badala ya malezi ya kuonyesha kuwa na Imani nao. Wakati huo huo, Wanaume wamewapa wanawake malezi kuonyesha kuwa na Imani nao, badala ya malezi ya kuwajali. Kutokana na mpishano huu, ndoa nyingi zimejikuta katika mivutano mingi, na changamoto ya kutokuridhishana, kwa pande zote mbili.
Utakuta, kwa vile mahitaji ya Mwanamke ya msingi ya hisia za moyo ni mwenzi wake kumjali, basi anafikiri ndiyo mahitaji ya msingi ya Mwanaume pia. Vivyo hivyo, utakuta Mwanaume anataka mpenzi wake aonyeshe kuwa na imani naye. Hivyo, anajaribu kutoa mapenzi ya kuonyesha kuwa na Imani kwa mwenzi wake hitaji ambalo yeye angependa apatiwe na huyo mwenzi wake. Kila mmoja, pasipo kujua, anatoa aina ya mapenzi ambayo yeye angependa apatiwe, badala ya mapenzi ambayo mwenzi wake angependa apatiwe, kutokana na tofauti ya kijinsia aliyonayo.
Kwa kuelewa tofauti hizi za jinsia, na kwa kujitahidi kuuweka ufahamu huo katika matendo, misuguano iliyoko katika ndoa kati ya wanawake na wanaume itaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Ingawa hii pekee yake haitoshi kumaliza mivutano na migogoro katika ndoa, lakini ni moja ya njia muhimu ya kuboresha mahusiano katika ndoa.
Kuna wanandoa ambao, hata pasipo ufahamu huu, wameweza kuchukualiana na kuishi pamoja kwa mafanikio, na kuweza kuoanisha tofauti hizi za kijinsia. Hii ni kutokana na kipawa na alichonacho mmojawapo au wote wawili, katika kuoanisha tofauti hizi. Lakini, kufanikiwa huku pasipokuwa na ufahamu huu kunatokana na kipawa cha kuzaliwa.
Lakini hata kama mtu anacho kipawa cha kuzaliwa, kukiboresha kupitia kuongeza ufahamu ni jambo la msingi. Hata kama ndoa ni bora, siku zote kuna nafasi ya kuzidi kuboresha zaidi na zaidi kupitia kuongeza ufahamu kuhusu ndoa. Maarifa siku zote ni silaha. Yaani maarifa yanampa mtu uwezo wa kutawala jambo.
Maarifa, ufahamu, ujuzi au elimu ni silaha muhimu sana kwa binadamu, silaha ambayo ikimpa kudhibiti mambo, na kutawala changamoto mbalimbali katika maisha yake. Na katika ndoa pia, maarifa yanayohusu ndoa ni moja ya mhimili muhimu.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU