Unapofanya kitu chochote kwa mtu yeyote fanya kama unajifanyia wewe pasipo #kutegemea chochote kutoka kwa mtu huyo.
Kinachowaumiza watu wengi ni #matarajio ambayo wanakuwa wameyaweka wakiamini watapata kutoka kwa watu baada ya kuwasaidia.
Ukiishi kwa kanuni hii "Chochote nitakacho mfanyia mtu nitakua nimejifanyia mimi" hautachoka kutoa msaada kwa watu, kinachosababisha watu wengi wavunjike moyo kusaidia ni ile kudhania kwamba kwa kusaidia labda #watakubalika, wataheshimika au watapata kitu fulani kutoka kwa waliosaidiwa, sasa baadae wanapokosa ndio chanzo cha uchungu ndani yao.
Kumtendea kitu kizuri mtu huku ukiwa unatarajia kitu kutoka kwake hiyo ni dalili ya ubinafsi.
Kumtendea kitu kizuri mtu huku ukiwa unatarajia kitu kutoka kwake hiyo ni dalili ya ubinafsi.
Maisha yenye furaha yanakuja katika kusaidia wengine pasipo kutaraji chochote kutoka kwao. Usiache kusaidia pale unapohitajika kusaidia, na usisaidie kwasababu unataraji chochote kutokana na msaada huo.
Umuinuapo mwenzako, umejiinua wewe.
UBARIKIWE NA BWANA. π