-->

AMRI KUMI ZA MAISHA YA NDOA… ⚠️🚫‼️


1. USIJITENGENEZEE MAHUSIANO MENGINE YANAYOZIDI MAHUSIANO YAKO NA MWENZI WAKO: Pasitokee MTU mwingine (wa jinsia yeyote) ambaye atakuwa na umuhimu wa juu zaidi kuliko mwenzi wako.
2. USIMLINGANISHE AU KUMSHINDANISHA MWENZI WAKO NA MTU MWINGINE: Kumbuka kila mtu yupo tofauti. Tumia hekima kumsaidia mwenzi wako kuwa bora zaidi pasipo kumfanya ajisikie kwamba hafai au hana viwango unavyotaka wewe.
3. USITUMIE “TENDO LA NDOA” KAMA FIMBO YA KUMWADHIBU MWENZI WAKO: Hata kama mmepishana misimamo, kumbuka “Tendo la Ndoa” ni haki ya msingi ya kila mwanandoa.
4. USIISHI MAISHA YA SIRI KWA MWENZI WAKO: Fanya jitihada za makusudi kuvunja kila tabia ya usiri ambayo itasababisha kila mmoja aishi maisha yake binafsi.
5. USIJILAUMU KUINGIA KWENYE NDOA AU KUMWONYESHA MWENZI WAKO KWAMBA UNAWEZA PATA MBADALA WAKE WAKATI WOWOTE ULE: Hata kama unahisi “ulichemsha”, sasa fanya wajibu wako kuiboresha hiyo ndoa. Kumbuka UPENDO una nguvu kuliko MAUTI.
6. USIRUHUSU KAZI AU MAJUKUMU YAKO YAIDHOOFISHE NDOA YAKO: Pamoja na majukumu mengi uliyonayo, hakikisha umuhimu wa ndoa yako unabaki palepale.
7. USIWE MBINAFSI: Usipendelee mambo yako tu au ndugu zako tu; bali kumbuka pia mwenzi wako anao upande wake.
8. USIWE MWEPESI KUSAMBAZA MAMBO YENU YA NDANI KWA KILA MTU: Ndoa ni taasisi yenye kanuni na taratibu zake; mojawapo ya kanuni hizo ni “utunzaji wa mambo nyeti” (Confidentiality). Uwe makini unamwambia nani, kitu gani, wakati gani, na mazingira yapi.
9. USIJIDANGANYE KWAMBA KUNA MTU MWINGINE ANAKUPENDA NA KUKUJALI ZAIDI YA MUME/MKE WAKO: Kumbuka kuna watu wataonyesha wanakujali sana kwa sababu sasa upo kwenye ndoa; siku ukitoka hutaamini kama ndio wale!!
10. USISAHAU KIAPO CHA NDOA NI KIAPO CHA DAMU… NI KIAPO CHA MAISHA: Usiruhusu mawazo ya kutengana au kuachana yawe RAHISI na MEPESI sana ndani ya kichwa na moyo wako. Mara zote katika changamoto jikumbushe KIAPO CHA NDOA… “Nitakuwa nawe katika hali zote…!!”
NB:
💥 Paleka shida zako kwa MUNGU kabla hujazipeleka kwa MARAFIKI au WAPAMBE.
💥 Msaidie mwenzi wako kwa UPOLE na UVUMILIVU awe jinsi ambavyo ungependa awe.
💥 Usitumie KINYWA au MANENO yako kuilaani NDOA yako… bali tamka BARAKA katika ndoa yako.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU