Mume mwema ni mtu tofauti kabisa; namna anavyoishi na mkewe humfanya kuwa tofauti na wanaume wengine.
Kuna tofauti kubwa kati ya mume mwema na wanaume wengine, na anauonesha wema wake kwa njia zifuatazo:
1. KAMWE HAKULINGANISHI NA MWANAMKE MWINGINE
Mume mwema atakuthamini na kukupenda hivyo ulivyo; hukufanya uwe bora na haoni sababu ya kukulinganisha na mwanamke mwingine.
2. ATAKUWA MWAMINIFU KWAKO
Mume mwema hatoacha kuwa mwaminifu kwako; uaminifu ni kipaumbele chake. Hatoacha kulinda heshima yako na heshima ya ndoa yenu.
3. HAMVUNJII HESHIMA MKEWE
Mume mwema atakuheshimu; ataamiliana vyema na wewe, atakutegea sikio na kukufanya ujihisi kuwa wewe ni mtu muhimu kabisa katika maisha yake.
4. ATAKUFANYA UJIHISI MWENYE THAMANI
Mume mwema hatokufanya ujihisi kuwa huna thamani. Ukiwa na mume mwema, utakuwa na uhakika wa penzi lake kwako na utakuwa na uhakika kuwa kweli anakuthamini.
5. HATOKUFANYA UJIHISI KUWA NI MPWEKE KATIKA NDOA/ UHUSIANO WAKO
Mume mwema hatokufanya ujihisi mpweke katika ndoa yako; atakufanya kuwa sehemu ya ndoa yenu, na utajihisi kuwa ndoa yenu inakuhusu pia.
6. HATOKUFANYA UJIHISI KUWA HUMRIDHISHI
Mume mwema atakufanya uhisi kuwa unapendwa; ataridhika kuwa nawe katika maisha yake. Ukiwa na mume mwema, hutojihisi upungufu, hutojihisi kuwa wewe ni mbaya, hutojihisi kuwa hupendwi --- atakufanya ujihisi kuwa wewe ndio kila kitu kwake.
7. HATAKUPIGA NA KUKUUMIZA.
Mume mwema atauchukulia mwili wako kama mwili wake; hatothubutu kukupiga mpaka akuumizs, hata akiwa na hasira kiasi gani. Hatoitumia hasira yake kama kisingizio cha kumpiga mkewe. Anakuthamini na anauthamini mwili wako pia.
8. HATOKUTUKANA
Mume mwema kamwe hawezi kukufedhehesha au kukukebehi; kamwe hawezi kukuumiza kwa kauli za kinywa chake.
HITIMISHO
Hizi ni baadhi ya faida za kuwa na mume mwema. Mume mwema hatokufanya ujihisi kuwa wewe ni duni, kupitia kauli zake na matendo yake.
Nakutakia ndoa yenye furaha..