-->

MWANAMKE JIFUNZE JINSI YA KUISHI NA MUME.NA UKAIFURAHIA NDOA YAKO KILA SIKU


Kazi ya mke ni kumtunza na kumlea mume, Si kazi rahisi Wanawake ambao hawatambui sifa hii ya wajibu wao, wataona vigumu katika kutimiza kazi hii.
Ni kazi ya mwanamke ambae anatambua kwamba kazi hii inahitaji kiwango fulani cha busara, mtindo na ustadi.
Kwa mwanamke kuwa mke aliyefuzu, lazima auteke moyo wa mume wake na kuwa chanzo cha furaha kwake.
Lazima amtie moyo katika kutenda matendo mema na kumshawishi asifanye matendo maovu.
Lazima pia mke achukue hatua za kutosha kutunza afya yake na ustawi wake.
Matokeo ya bidii yake yanaelekezwa katika kumfanya mume awe mwema na anaye heshimika ambaye atastahili kuwa mlezi wa familia yake, na baba mzuri ambapo watoto watapata mwongozo na heshima.
Mwenyezi Mungu na Mjuzi wa yote amemjaalia mwanamke uwezo usio wa kawaida. Mafanikio na furaha, na pia mateso ya familia yapo mikononi mwake.
Mwanamke anaweza kuifanya nyumba kuwa pepo ya hali ya juu au jahanamu inayowaka moto.
Anaweza akamfikisha mume wake kwenye kilele cha mafanikio au balaa isiyofaa.
Mwanamke mwenye sifa alizopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, ambaye anatambua wajibu wake kama mke, anaweza kumnyanyua mume wake kuwa mtu wa kuheshimika hata kama alikuwa mtu wa chini sana kuliko wote.
Wanawake wanao uwezo wa ajabu ambao kutokana nao wanaweza kupata chochote wanachotaka.
Mwanamke anayemtii mumewe amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi.
Ndugu zangu katika iman tujitahidi saana wanandoa kuvumiliana, kama hatuna uvumilivu ndoa haiwezi kudumu.
Tujitahidi sana kwa hili kwani kila mwanadamu ana mapungufu yake tuvumiliane ili ndoa zetu ziweze kudumu.
Mwanaume huwezi kumpata mwanamke aliyekamilika kila kitu na wala mwanamke huwezi kumpata mwanaume aliyekamilika kila kitu.
Kikubwa zaid ni kuvumiliana na kuelekezana!!
Share:

Related Posts:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © 2025 UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU