-->

MBINU NYEPESI NA RAHISI KABISA MKE ANAZOWEZA KUZITUMIA KUMTEKA MMEWE KIAKILI

Image may contain: 2 people

Limbwata na juju kamwe haviwezi kuwa dawa ya kumteka mwanaume kiakili na kumdhibiti katika ndoa, HUO NI UCHAWI TU. Mapenzi yanahitaji ufundi wa hali ya juu ili kumfanya uliye nae asishawishike kujaribu michepuko , sawa huwezi kumpa kikamilifu ila waeza kumpa maradufu kiasi cha kumfanya aamini mambo yote mazuri yapo ndani ya ndoa tu. Mwanamke zingatia haya machache marahisi kabisa hakika mmeo hatokaa atamani kuchepuka:

1. MAPOKEZI
Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yake yoyote ile, anza kwa salamu nzuri. Mpokee na kumkumbatia huku uso ukiwa na tabasamu la bashasha.
2. MAVAZI
Jipambe na upake manukato kwa ajili yake mpenzi wako. Vaa vizuri nguo ziwe za kuvutia zenye heshima na hadhi ajiskie hamu hata ya kutoka out au kuongozana na wewe. Jitahidi kuvaa zile alizokununulia yeye kama zawadi maana huwa hizo hu reflect mavazi unayompagawisha zaidi ukiyavaa.
3. USAFI WA MWILI.
Ili kumteka akili mumeo inatakiwa ujue kuoga vizuri na ujue kujiweka safi mda wote sio unanuka vijasho vya ajabu ajabu. Usafi utawale maisha yako mwilini, akilini, tabia mpaka kitandani.
4. JUA NAMNA YA KUZUNGUMZA NA MUMEO
Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka atakapopumzika ndio umuambie.
5. SAUTI
Pendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo kuongeza nakshi katika masikio yake… usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine ni mwiko.
6. MTINDO
Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika. Lakini usizidishe kiwango na ufanye hivyo kwa mumeo tu.
7. MAHANJUMATI
Mpikie chakula kitamu ajirambe maana waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea.
Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi huwa wanajali ladha tu. Mpe mapishi matamu ili kumfanya akumiss pale anapokosa huduma yako.
8. SHUKURU
Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.
Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: “Kwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?” Epuka hali hiyo.
9. HESHIMA NA UTIIFU
Daima kuwa mtiifu kwa mumeo pia uwe mwaminifu kwa kipenzi chako.
10. Muunge mkono kupitia kazi yake, fedha yake au mali yake pindi inapohitajika. Japo hii wanawake wengi hushindwa kufanya hivyo.
11. MAAGIZO.
Fuata maagizo yake, isipokuwa katika mambo ya haramu katika Uislamu/Ukristo, mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na ni mshauri wake.
12. EPUKA
Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha mumeo/mpenzi wako.
Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.

13. Zaidi ya sana hakikisha unamzoesha kusali sala na kusoma maandiko matakatifu ambayo yatamjenga kuwa na HOFU YA MUNGU pia yatasaidia kukuepushia majanga mengi yasiyo ya lazima ambayo iwapo asingekua mtu wa ibada angeyashiriki ikiwemo ulevi, uzinzi, uchawi, utapeli, wizi, ushoga, ugomvi na mambo mengine maovu. Hii ni mbinu kuu na ndio lengo langu siku ya leo kuwa ndoa sio kitu pasipo uwepo wa ibada ya kweli na hofu ya Mungu, ombeni na msali pamoja Mungu awabariki katika maisha yenu aibariki familia yenu na kuilinda.

Kama umenielewa TYPE "AMEN"

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU