-->

EPUKA KUWA CHANZO CHA MAUMIVU, MAJUTO NA MAJONZI KWA MTU AKUPENDAE

Image may contain: 1 person

#inasikitisha sana

Thamani ya upendo wa dhati kwa akupendaye imejificha katika udhaifu wake kwako maana kutokana na upendo wake wa dhati kwako hujikuta amekufa ameoza yaan hujishusha na kukupa nafasi ya wewe kumtawala yaan unakua kama King au Queen kwake hivyo chonde chonde epuka kuitumia heshima hiyo unayopewa na akupendae kumsababishia maumivu na majonzi INAUMA SANA.

mkeo, mmeo au mpenzi wako anapokiri kuwa anakupenda sio kuwa yeye ni dhaifu au haoni wengine bali ameamua kukuchagua, amekukubali, amekuridhia, amejitoa kwako, amekuheshimu kuliko wote, amekupa maisha yake na moyo wake, amekuamini hivyo ACHA NYODO.

Huenda ukamuelewa vibaya na kumuona CHEAP ila kabla hujafikiria hivyo jaribu kuuliza wa nje marafiki na jamaa wanamtazamaje ndipo utapogundua wewe ndio mdhaifu maana unampuuza ila wengine wanamtamani na kummezea mate wakitamani siku moja muachane wamdake, hata ng'ombe huwa anaudharau mkia wake ila siku ukikatwa ndio anajuta kuupoteza MTHAMINI AKUPENDAE.

Mapenzi ni hisia, ukiona mtu amekubali kuwa nawe maana yake amekupa dhamana ya kuzipalilia hisia zake na kumtuliza hivyo chonde chonde epuka kuwa mzigo na msiba moyoni mwake, inauma sana mwanzoni ulipomhakikishia kuwa unampenda sana pia alafu leo unamgeuzia kibao unachepuka na wapenzi wengine hujali hata ahadi zenu huogopi hata UKIMWI hakika huna tofauti na shetani kwa kuwa uasi ndio tabia yake, BAKI NJIA KUU.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU