-->

#BINTI:ULIOMBA SANA MUNGU KUOLEWA, NDOTO IMETIMIA ITUNZE, IFURAHIE, IENZI NDOA YAKO, EPUKA YANAYOHATARISHA UHAI WA NDOA YAKO.

Image may contain: 1 person, smiling

Majuto na vilio vya kujitakia huja pale unapojisahau na kuzichezea hisia za mtu aliyekupenda kweli na kukuoa uwe mke wake, anapokuoa wewe haina maana kuwa hajaona au haoni wanawake wengine warembo kuliko hata wewe ila tu moyo wake umeamua kukuchagua wewe na kukukabidhi hiyo heshima ya kuwa mama wa watoto wake, ILINDE. Usiruhusu moyo wako kumdharau aliyekuoa ukamuona kwako ndio kafika hivyo hatoweza kufurukuta hata ukimfanyia maudhi na vitimbi hakika nakuhakikishia ipo siku UTAACHWA KWA AIBU KUBWA SANA maana akili zetu wanaume twazijua wenyewe.

Binti uliyeridhia kuolewa na kuwa mama wa familia yako ya nini kuendelea kutamani asivyo navyo mmeo? Kwanini unapokea vizawadi zawadi vya wanaume wengine eti kisa marafiki, majirani au classmates wako wa zamani? Kwanini unachati chati na kutumiana vimeseji na marafiki zako wa zamani wa kiume hata kama sio kwa ubaya? Kwanini unathubutu kuwatembelea rafiki zako wa zamani au majirani au wafanyakazi wenzako wa kiume bila hata kuambatana na mme wako? aisee naona haujajua BOMU unaloliandaa hakika mlipuko wake utajikuta umeachwa kwa aibu mno. Hapa namaanisha ukiwa mke wa mtu epuka mawasiliano na ukaribu wowote na marafiki au majirani au wafanyakazi wenzako wa kiume ili kuepusha hatari zisizo za lazima kwa ndoa yako.

Mwanaume aliyekuoa amefanya maamuzi yake ya maisha akiamini sasa hatokaa vijiwe vya mabachelor na kushiriki story za mademu na kula bata bali ataanza kujiunga na wazee wazoefu katika ndoa na kupata maarifa zaidi ya kuwa baba bora na namna ya kulea familia yake yaani wewe mkewe na watoto wenu ila sasa kwanini wewe binti bado unawaza mitindo ya nguo, vipodozi vipya, shopping, club, out, iPhone note 7, Samsung Galaxy na mambo ya kijinga wawazayo mabinti wanaobalehe???!.... Dah napata hasira sasa, please wewe sasa ni mama wa familia anza kuwaza ni jinsi gani uwatunze watoto wako utaozaa na mmeo ili wakue katika njia iliyo bora, waza ni jinsi gani unaweza kumshauri mmeo mkajenga, mkaanzisha miradi, mkaboresha maisha yenu na mambo mengine ya msingi kuhusu familia maana sasa sio mda wa kujifikiria binafsi na tamaa zako kwa kuwa ndoa imewafanya mmekua MWILI MMOJA hivyo yote mpangayo na kuyawazia yawe yenu nyote pamoja na Mungu awabariki katika maisha yenu ya ndoa. Ailinde familia yenu awape mafanikio, amani na baraka tele.

Uliye katika ndoa au unayetarajia kuingia katika ndoa, kama nimekugusa kupitia ujumbe huu hakikisha una Comment niambie umejifunza nini kisha SHARE post hii na marafiki zako nao wajifunze.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU