-->

JE! NI KWA NINI NDOA ZA MABABU ZETU ZILIDUMU MNO PASIPO KUVUNJIKA???!!!.

.No photo description available.

Miaka hii imekua ni jambo la kawaida kushuhudia ndoa iliyofungwa mwezi November ikivunjika December, yaani ikifika January watu washaisahau na tayari wale walioachana kila mmoja tayari yupo katika mahusiano mapya na mpango wa ndoa mpya. Hii inaonesha ni kiasi gani vijana miaka hii wanaingia katika ndoa KIMIHEMKO yaan hawapo serius maana ndoa kama hiyo imevunjika ndani ya mwezi mmoja na tayari waliotengana wana wachumba wapya jiulize JE! KULIKUA NA MAPENZI YA KWELI HAPO?? !! au ni usanii mtupu na kuzugana??!!.

Wazee wetu enzi zao walikua serius mno na suala la NDOA ndio maana ndoa zao zilikua hazivunjiki mpaka labda kifo kiwatenganishe. Familia zao zilidumu kwa amani, furaha, umoja, upendo na undugu ambapo wapo waliokua wakifikia kuadhimisha JUBILEE za miaka hadi za miaka 50 ya ndoa zao, Hahahahahaaaaaa ila miaka hii utakuta watu wanaadhimisha miezi 6 ya ndoa yao maana wanajua kuumaliza mwaka ni shughuli pevu.

Tuangalie kwa kina je ni mambo gani hasa yalisababisha ndoa za mababu zetu kudumu?
1) NIA YA DHATI
Walikua wakiingia kwenye ndoa kwa mipango thabiti na nia, walikua hawaoani kisa mimba, upweke, umri, kuiga, agizo la wazazi au hamu ya tendo la ndoa. Siku hizi hizo ndio sababu za vijana wengi kuoana hivi unafikiri kwa sababu hizo ndoa zitadumu kweli???

2)UAMINIFU
Walikuwa na viapo vikali vya kimila walivyovitii na kuviogopa ambavyo viliwabana kuhusu USALITI hivyo walizilinda ndoa zao kwa umakini, waliaminiana na kuishi kama mwili mmoja. Miaka hii utakuta mme /mke hataki hata mkewe au mmewe athubutu kugusa simu yake maana ni mwendo wa michepuko na usaliti, ikiguswa hiyo simu mtu anajaa povu inakuwa ni Ugomvi mkubwa, ndoa itadumu kweli hapo?????

3)UPENDO WA DHATI
Wazee wetu walipendana kwa dhati yaani baada ya kuoana mme alifunga macho na kumuona mkewe ndio kila kitu vivyo hivyo mke nae. Walipendana wakavumiliana, wakashauriana, wakasaidiana, wakafarijiana, wakaongozana na kushirikiana yote ya muhimu ili kujenga ndoa na familia zao. Siku hizi ndani ya ndoa nyingi kila mtu mke na mume wanafanya mambo yao kwa siri eti SURPRISE mwisho wa siku USALITI unaivunja ndoa bila kusahau migogoro na chuki.

Hayo ni baadhi ya mambo ya muhimu yaliyosababisha ndoa za mababu zetu kudumu, nitaongeza mengine siku nyingine kwa leo naishia hapo.

Kama umenielewa comment chochote kisha SHARE post hii na marafiki zako wapate funzo hili.

Hii post ni dedication kwa wazazi wangu Mama yangu Josephina William na Baba yangu mzee William masawe, Mungu awabariki.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU