Wasichana wengi mmekuwa na kilio kikubwa sana kuhusu mahusiano yenu, na mnadai hamna imani na wanaume kabisa, jambo ambalo ni hatariiiiiii sana, sasa hebu tuangalie jambo moja hapa.
Kila siku nipo nanyi nikijaribu kutafakari jinsi gani niwasaidie ili pengine kunusuru hali ngumu za mahusiano, lakini leo ninalo jambo kwenu.
Kwa siku hizi kadhaa nimejifunza kwenu jambo ambalo sijaweza kukaa nalo, nimeona Ngoja niwaambie hapa hapa kabla hamja haribikiwa.
Najua wanawake wengi mnaomba Mungu awape waume wema lakini ninyi hamko tayari kuwapokea hao wanaume wema, mnatumia akili zenu kupata waume ambao mwisho hawawafai mwisho mnalalamika na kuwadharau wanaume wote na wasio na hatia.
Mfano kuna wanaume ni wapole, wanajua thamani ya Mwanamke, wanajali na ni wenye hekima, wanajua mtahitaji ya Mwanamke, ni wacha Mungu, wanajua kubembeleza kwa maneno safi, na ni wepesi kuhifadhi madhaifu ya Mwanamke. Lakini wanaume hawa unakuta hana uwezo mwingi kifedha. Nimesikitishwa sana kuona kuna wanawake au Mabinti wengi kuona mkidai na kuhoji kwamba tena kwa dharau kuwa et
je Mtakula hayo maneno matamu?
Je, maneno yake ya upole yatawapeleka saloon?
Je, upole wake utakuwa chakula?
Mkimaanisha kuwa hayo hayana thamani kwenu, ila zaidi sana Mwanamume mwenye pesa ndiye mwenye tija kwenu.
Mnataka Wanaume wenye pesa, wenye uwezo wa kuwapeleka saloon, wa kuwapa chakula kizuri, kuwalaza pazuri, kuwapa nguo nadhifu nk. Lakini mwisho Wanaume hawa hawajali uwepo wa mke, hawajui kushuka kwasasabu ya kiburi cha pesa zao, wanawawatelekeza na mwisho mnaanza kuwadharau Wanaume wote wakati wengine mnawaonea tu.
Mwisho ndio maana hata maombi yenu yanaonekana hayana maana, mkiomba Mungu anawapatia lakini wakifika hao wanaume wema, mnawapima kama wanaweza kuwahudumia, kama hawana mnawakataa maana yake umekataa chaguo la Mungu kwako ila unaingia kutafuta mwenyewe unayeona atakufaa kwa kigezo cha mwenye unafuu wa maisha.
Upendo wa dhati unaficha madhaifu yenu ndani, pasipo upendo pesa ya kazi gani?
Anakupenda na hana uwezo basi mpokee na umpe ushirikiano kisha msaidiane kutafuta maisha, mnataka maisha yaliyo andaliwa na nani?