-->

KWENYE MAPENZI MUOGOPE SANA MTU MWENYE MITAZAMO HII

Image may contain: 1 person, smiling, standing and outdoor

Muogope sana Mtu ambaye yeye mwenyewe mtazamo wake umekomea kuamini kwamba PESA💸 GARI🚘 NYUMBA🏰 SHAMBA MTOTO AMA WATOTO👪 pamoja na SAMANI za nyumbani kwake ni FAHARI YAKO.
Yaani namaanisha kwamba unakutana na Mtu kwa sababu anaona anakutimizia MAHITAJI kwake ni siraha🔫 ya kukumaliza ki akili eti uone zaidi ya hapo unataka nini🙍
Tatizo hilo lipo kwa watu ambao wao hujiweka kwenye mamlaka ya UTAWALA Yaani badala ya kuitafuta FURAHA YA MAPENZI wao hujikita kwenye;
"KUMPUMBAZA MWENZA WAKE ILI AONE BILA YEYE HAWEZI KUMPATA WA KUMJALI HIVYO"
Nafikiri huo ni UJINGA kabla haujawa ushamba, Mapenzi sio chakula, Maradhi mazuri, Kutembelea gari, Wala kuwa mvaaji wa kila toleo, Ingekuwa maradhi mazuri ndo ULINZI WA PENZI wanaokutanaga machakani wasingefurahia penzi lao na pengine ni TAMU kuliko la mnaolala kwenye 6×6
Kama chakula kingejenga PENZI hujiulizi kwa wanaokula TEMBELE na wako na AMANI TELE?
Ni gari ndilo unafikiri limemtuliza MKE? Kwani hujui masikini ndo wanafurahia zaidi PENZI kuliko wenye navyo?
Nguo ni sehemu ya kusitiri mwili labda na kuleta muonekano tu zaidi ya hapo wala hazina kazi Kwani ingekuwa NGUO husababisha PENZI kuimarika hujiulizi wana mitindo nao wanahangaika kutetea mahusiano yao? Kwani wao ndo hubuni matoleo ya mavazi, Zaidi ya AMANI wala hayo hayana nafasi kwenye NAFSI.
Ukitaka kujua kwamba MAPENZI NDIYO DIRA YA FURAHA YA MWANA WA ADAM YEYOTE Kwanini Mtu akiyakosa MOYO HUUGUA?
Kataa kuwa MTUMWA kisa ya UMASIKINI wako, UMASIKINI ni akili wala sio Mali Kwani Kuna aliyezaliwa na nguo?
Sote tumezaliwa UCHI! Ndo maana halisi ya kwamba;
"KILA MTU ANATAKIWA KUTUMIA AKILI YAKE KUWA NA VITU KWA SABABU AKILI NDIYE DEREVA WA KILA KITU"
Unafikiri ni kwanini PUNGUANI "kichaa" Hajui KUTOFAUTISHA KATI YA UCHAFU NA USAFI? Kwa sababu akili haijatimia, Unaweza ukiamua, Hutafanikiwa ikiwa umetawaliwa, UTAFIKIA MALENGO YAKO IKIWA NYUMA YAKO HAUKO NA MTU MBINAFSI Kwani wengi wameharibiwa maisha yao kwa kukosa wenza wema, MAPENZI NI NJIA iendayo kwenye FURAHA lakini
pia inaweza kukupeleka kwenye MAJUTO🙇
Fikiria zaidi kabla ya KUZAMA PENZINI kwa sababu MOYO hupenda ila unajua kuugua na ukiugua UMEITESA NAFSI.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria💓
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU