-->

KUNA MITAZAMO TOFAUTI MWANAMKE NA MWANUME ANAPOTOKEA KUMPENDA MMOJA WAO HASA ANAPOTAKA KUINGIA NE KWENE MAHUSIANO MAPYA.

Kuna mitazamo tofauti mwanamke na mwanaume anapotokea kumpenda mmoja wao..hasa anapotaka kuingia nae kwenye mahusiano mapya..
Kwa mwanamke...
Wengi utumia hisia sana kumuelewa mwanaume kuliko akili na ndio maana ni ngumu kufahamu tabia ya mtu mwanzoni anapotakwa.. Hii imewafanya asilimia kubwa ya wanawake kuingia kwenye mahusiano na watu ambao sio sahihi kwao
Kwa mwanaume...
Asilimia kubwa pamoja na kuangalia muonekano wa nje wa mwanamke lakini ukweli ni kuwa kama anampenda mwanamke anaetaka kuingia nae kwenye mahusiano ya kimaisha mara nyingi uchunguza tabia ndogo ndogo za mwanamke huyo kuliko anavyotazama muonekano wake na ndio maana mwanaume anaweza kutembea na wasichana warembo sana akaenda kuoa mwanamke ambae sio mrembo sana kuliko wale aliowahi kutembea nao... Hii inamaana kwa sehemu kubwa wakimtaka mtu wa maisha yao utumia akili sana kuliko hisia.
Mwanamke ambae utumia akili kutaka kuingia kwenye mahusiano umchukua muda mrefu kuingia kwenye mahusiano maana japo hisia zipo kwa mtu yule lakini once akili yake inapomwambia jipe muda kumfahamu mtu huyu hawezi kumkubalia mwanaume kirahisi ... Atakukubalia mpaka pale atapoona akili yake imepunguza kujiuliza maswali kuhusu mwanaume anaemuhitaji ...na hawa ndio mara nyingi uingia kwenye mahusiano na watu ambao kwa sehemu kubwa ni sahihi kwao.
Hivyo uzuri na muonekano wa mwanamke huotoshi kukufanya ukapendwa kweli .. Vile vile mwanaume kumtamkia mwanamke maneno ya kumkamata hisia zake anapokuwa anamtaka kimahusiano sio garantii ya kuwa kweli anampenda ...
Ili muwe na uhakika na kile mnachokitaka ni vema mkapeana muda wa kujuana kuliko kuwahi kuingia kwenye mahusiano
Dayari Yangu
Image may contain: 2 people, people standing
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU