Ukweli ni kwamba kama ilivyo kwenye biashara, kuna wakati tunakaa na kujadili nini cha kufanya ili kuwa na biashara iliyo imara, tunapaswa pia kupata muda wa kukaa na kutafakari hali ya uhusiano wetu.
Ukinichukia wewe, haimaanishi kwamba siwezi pendwa na watu wengine. Wanaume wengi wanashindwa kutembea na wake zao kwa sababu hasa ni kwamba wameshawafuja kiasi kwamba hawana mvuto tena, kama walivyokuwa nao wakati ule wanawaoa.
Unapokuwa na ndoa mbaya, usianze kulaumu, bali tafakari kwa makini. Wengi wanaharibu wenyewe ndoa zao, kisha wanatafuta wachawi.
Ndoa inapokuwa nzuri, fikra za wahusika zitakuwa ni namna ya kuimarisha uhusiano wao na kuwasaidia watoto wao wawe na maisha bora zaidi.
Kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa na wanasheria wa familia ni muhimu kuwa na watu au mtu utakayekuwanaye katika mazungumzo ya namna ya kuimarisha uhusiano wako.
Kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa na wanasheria wa familia ni muhimu kuwa na watu au mtu utakayekuwanaye katika mazungumzo ya namna ya kuimarisha uhusiano wako.
Kuharibu uhusiano, kunaharibu mambo mengi katika maisha. Kwa mfano kulingana na sheria za ndoa, itakupasa mgawane mali, kuwasumbua watoto (kwa wanandoa ambao tayari wana watoto), kuwa na ugumu wa kuoa au kuolewa hasa kutokana na ukweli kuwa siyo Wanaume au Wanawake wengi wanapenda kuoana na wanawake ambao tayari wamezaa...unaanza kuitwa baba au mama wakati bado hujazaa naye❗
Sababu kubwa ya watu kuogopa kuoana na mtu ambaye tayari ana mtoto au watoto hasa ni woga na kuwa Baba au Mama watoto anaweza kuja baadaye kuangalia watoto au mtoto.
Kwa baadhi ya watu wasio na msimamo huweza kuanzisha uhusiano upya hata kama ni kwa siri.
Kwa baadhi ya watu wasio na msimamo huweza kuanzisha uhusiano upya hata kama ni kwa siri.
Ndugu zangu, nimezungumza mengi lakini, ninachotaka kukisisitiza ni kwamba, mchawi wa penzi lako ni wewe mwenyewe...❗ Ni lazima uwe makini kwa kile unachosema au kutenda kwa mwenzi wako.
Kuna idadi kubwa ya Wanandoa, kwa kutenda au kuzungumza kwao, ama kwa kujua au kutojua, wamekuwa wakisababisha wenzi wao kuwachukia..
Hapa nazungumzia kwa wachumba na wanandoa. Kuna watu baada ya kuishi pamoja kwa miaka mingi huanza kudharauliana, jambo ambalo siyo zuri katika maisha.
Hapa nazungumzia kwa wachumba na wanandoa. Kuna watu baada ya kuishi pamoja kwa miaka mingi huanza kudharauliana, jambo ambalo siyo zuri katika maisha.
Unamchukuliaje Mkeo❓ Mimi sijui unavyoishi na Mkeo, lakini ukweli ni kuwa tafiti zinaonyesha kwamba, kama humweshimu Mkeo, tegemea kuwa iko siku atatoka nje ya Ndoa, hata akiwa ni mtu mwenye kujiheshimu kiasi gani .
Watu wanaoana siyo kwa sababu wanatafuta fedha au wanatafuta sehemu ya kula lah, wanatafuta kupendwa. Hivyo, kama wewe huonyeshi upendo kwa Mkeo, tegemea kupambana na mabaya.
Je, Mkeo unamchukuliaje❓ Ni sawa na thamani za ndani ya nyumba yako....kama meza, kabati, sufuria au❓ Mimi sijui, ila jibu unalo. Ninachotaka kukusisitizia ni kwamba, kwa namna unavyoishi na mwenzi wako, unamfanya awe mbaya au mzuri kwako.
Je, Mkeo unamchukuliaje❓ Ni sawa na thamani za ndani ya nyumba yako....kama meza, kabati, sufuria au❓ Mimi sijui, ila jibu unalo. Ninachotaka kukusisitizia ni kwamba, kwa namna unavyoishi na mwenzi wako, unamfanya awe mbaya au mzuri kwako.
Je, wewe Mke unamchukuliaje Mumeo ❓
Kama jitu jinga au unayepaswa kumpenda❓
Mumeo hana kauli juu ya uhusiano na mahaba❓
Kama jitu jinga au unayepaswa kumpenda❓
Mumeo hana kauli juu ya uhusiano na mahaba❓
Angalia kwa makini, kuna matendo ukifanya ni sawa na kumuuza mwenzi wako aende kwa wengine kusaka furaha unayomnyima.
Kama mmekubali kuoana, yanini kusumbuana❓ Yanini kunyimana na kuwekeana masharti mara ooh nimechoka, mbona jana tu tulinahii na leo unataka tena kwani mimi ng’ombe, aaah bwana eeeh kama ndoa yenyewe ndiyo hivyo, ni bora tuachane...❗
Ndivyo baadhi ya watu wamekuwa wakitoa kauli chafu, badala ya kubembelezana.
Ukishaolewa au kuoa, huna mamlaka ya kumzuia mwenzi wako kufanya anachotaka juu yako...ukifanya hivyo unajihatarishia mwenyewe ndoa yako. Ni kumwambia nenda kwingine ukapate unachotaka. Kwa nini unakuwa hivi ndugu yangu❓
Mpe nafasi mwenzi wako kufurahia uwepo wako, acha lugha kali na chafu...siku zote penda amani, penda kushuka hasa kama utaona hakuna athari ya kufanya hivyo.
Ni wazi hata kama mwenzi wako ana vituko kiasi gani, wewe ukijipanga vizuri namna ya kumpenda, uhusiano wenu unaweza kuendelea, watu wanachohitaji ni amani ya kweli kutoka kwa wenzi wao.
Kama mmekwaruzana, endeleeni kuwasiliana, kadiri mnapokuwa pamoja au karibu, mnaondoa uwezekano wa kuachana, mkiwa mbali mnaruhusu mambo mabaya kuingia. #Chunga_sana_NDOA_yako. Maana Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏 MAANA WAASHERATI NA WA-ZIN-ZI MUNGU ATAWAHUKUMIA adhabu Waebrania 13:4) malazi yawe Safi ni pamoja na kinywa chako