-->

HIVI UNAJUA KWAMBA LOLOTE LINALOTOKEA KWENYE MAISHA YAKO HUWA LINA MAKUSUDI YAKE.

Traditional Nigerian Wedding - Home | Facebook

Chochote kinachokuja katika maisha yako kimekuja kukusaidia, haijarishi ni kibaya au kizuri lakini lengo ni kukuinua wewe kutoka viwango vya chini kwenda viwango vya juu zaidi.
Katika jaribu ndimo kulimo kuinuliwa, jambo hili tunaweza tukaliona katika Biblia kwa ndugu zetu watumishi wa Mungu Ayubu na Daniel. Majaribu yaliyo wapata wapendwa hawa kwa macho ya kawaida yalionekana yamekuja kuwadidimiza kabisa lakini mwisho wa siku waliinuliwa na mpaka sasa ulimwengu unawakumbuka kama mashujaa wa imani.
Jaribu unalopitia sasa msomaji wangu halikuja kwako kukuzamisha au kukuondoa kabisa kwenye ramani ya ushindi, bali limekuja kukuinua na mwisho wa siku likufanye kuwa shujaa. Sasa basi badala ya kuliangalia jaribu hilo kama kikwazo anza kuliangalia hilo jaribu kama nafasi ambayo umepewa kama maandalizi ya ushindi, anza kuliangalia kama fursa ya kuitumia kufanya kitu bora zaidi.
Kitu kikubwa ninachokimaanisha hapa ni kwamba: Chochote kinachokuja katika maisha yako kiangalie katika hali ya uchanya.
Usikimbilie kuangalia wapi ubaya wa kitu ulipo, anza kwanza na wapi uzuri wa kitu hicho ulipo.
Usikimbilie kuangalia wapi tatizo hili limenikwamisha, anza kwanza na kuangalia nimefaidika vipi kutokana na tatizo hili.
Usikimbilie kuangalia hasara au maumivu uliyoyapata kutokana na kumpoteza mtu fulani katika maisha yako, anza kwanza na kuiangalia faida uliyoipata (mfano, fundisho) kutokana na mtu huyo kuondoka katika maisha yako.
Usikimbilie kulaumu na kukata tamaa kutokana na biashara yako kuzama, kimbilia kutafuta ulipokwama ni wapi ili uanze upya kwa nguvu zaidi.
Usikimbilie kuumia kutokana na kufanya vibaya katika masomo yako, anza na kuiangalia sababu ya kupata matokeo hayo na hatua za kuchukua ili ufanye vizuri zaidi.
Badala ya kuendelea kumsema mwenzako vibaya, anza kuiangalia faida unayoweza kuipata katika mtu huyo akiwa hivyo hivyo alivyo.
Tembea na hili: Kila kinachokufikia katika maisha yako kimekuja kukusaidia, yeyote anayekuja katika maisha yako anacho kitu cha kukusaidia. Usiwe mwepesi wa kulalamika au kukata tamaa pale linapokutokea jambo gumu katika maisha yako. Ninacho kushauri uwe mwepesi wa kuangalia fundisho ulilolipata kutokana na jambo hilo, lakini mhimu zaidi kulifanyia kazi fundisho hilo.
______
UBARIKIWE NA BWANA. 🙏
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU