-->

🌹❤HII NDIO MAANA HALISI YA MAPENZI❤🌹

Image may contain: 2 people

Inapendeza mkiwa wapenzi responsible kila mmoja kwa mwenzake yani wakati wa shida mko pamoja na wakati wa raha mwafurahi pamoja hiyo ndio maana ya mapenz ya dhati na huo ndio utamu wake. Mapenzi hugeuka utumwa, mzigo, stress na shubiri pale mnapokua wapenzi ila kila mtu yuko bize kama mtandao wa ZANTEL.
Hivi inawezekanaje unasema unampenda wakati hadi leo hujamtumia hata sms ya kumtakia heri ya Christmas na mwaka mpya au unafikiri wanaomzunguka hawana namba zake, usipojituma kulinda shamba lako nyani na tumbili hakika lazima watakuibia mazao mwisho wa siku utajikuta shamba sio lako uliwalimia bure. Ni jukumu lako kuhakikisha uhusiano au ndoa yenu inakua mpya na tamu kila kukicha, ongeza vionjo, ongeza vizawadi ongeza vi surprise mapenzi ni upofu usipuuze zawad au maneno matamu unayomwambia umpendae hakika kama kweli nae anakupenda yatakua yanamuingia na kuitawala akili yake kama RING TONES 🎤🎤🎻🎧🎷🎺🎸

Inapotokea ukajikuta upo kwenye mahusiano au ndoa na mtu anaejua kupenda hakika maisha yako hutakua unasubiri Christmas na mwaka mpya ili kufurahi bali hakika furaha itakua sehemu ya maisha yako. Mbali na ubize wa kazi na majukumu mengine ila sio mbaya baadhi ya siku mkizitumia kutoka na kwenda kupumzisha akili na mwili eneo la tofauti mkapunga upepo na kubadilishana mawazo. Ni kitu cha pekee sana kama katika mtoko wenu siku hiyo ukimfanyia surprise umpendae japo kwa kizawadi cha pekee ambacho hujawahi kumpa hakika hatokaa akusahau na moyoni mwake utakua umejijengea kumbukumbu ya pekee, utamteka kisawasawa.
Ni sikukuu sahauni stress na yote yalopita, ni mda wa kufurahi na kumshukuru Mungu kwa kufikia kipindi hiki salama tunapoukamilisha mwaka. Upendo utawale sio leo tu bali ikawe upya wa kuondoa makovu yote ya mwaka unaoisha, ni mda wa kujipanga upya kisaikolojia kuanza mwaka mpya kwa style nzuri itakayowafanya mfurahie maisha yenu zaidi.
Wapo ambao hujisahau mno na kujua akishampata aliekua akimpenda na kumuoa au kuolewa nae basi amemaliza kazi ila ukweli ni kuwa ili kuipalilia ndoa au uhusiano wenu mambo yale yanayojenga mapenzi kati yenu yanapaswa kuenziwa ikiwemo kutoka out na kufurahi pomoja.

Maneno kama i love you so much baby, i miss you, am happy to be with you, am so glad for you n. k mwaka huu uliyamis kutoka kwa umpendae sahihisheni mlipokua mnakoseana mwakani yasijirudie makosa
Upendo utawale kati yenu siku zote kila mmoja amis uwepo wa mwenzio akiwa mbali, mkikutana amani na furaha vitawale hayo ndio mapenzi sio kila kukicha mna nuniana na kuchukuliana serious kama KURUTA😂😂😂😂😂

Imepenya..... Haijapenyaaaaa????!?
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU