-->

HARUSI NI VAZI, NDOA NI MAJUKUMU:


Kama unaolewa au unaoa kwaajili ya kupendezesha umati wa watu basi utaijenga ndoa yenye majuto na kukosa mvuto, Lakin kama unaoa au kuolewa kwa kutimiza agano basi ndoa yako Itakuwa na misingi Imara.
👉Harusi ni vazi na sherehe ya siku moja, lakini ndoa ni agano la milele. Kwann nasema harusi ni vazi. Nikweli utahangaika kukodisha gauni au suti kwaajili ya kufanikisha sherehe yako ya harusi lakin ukimaliza shughuli ile basi nguo hiyo hurudishwa ilipo kodishwa. Lakin ndoa ukifunga ni agano la milele hakuna mkodisho wala kuazima uwe tayari kupambana na kila hali utakayokutana nayo.
👉Harusi ni sherehe ya pongezi kwa watu wawili ambao wamefunga pingu za maisha tayari wamekubali kuishi pamoja, Harusi ni shughuli ya umati wa watu wengi na hufanyika mahali pa wazi na hadhara. Baada ya tafrija basi watu hao waliokula na kusaza wanaondoka na kuwaacha peke yenu, ndipo nyie wawili mlioungana mnayaanza maisha yenu ya ndoa, Hakuna mtu yeyote aliyekuja kwenye harusi atakuja kukusaidia majukumu ya ndoa labda salamu pekee.
👉Ndoa ni agano la muunganiko wa watu wawili walioamua kuishi pamoja kama mume na mke ili kuijenga familia ya baba na mama. Ndoa ni majukumu na majukumu hayo yanatokana na umoja wenu, Mwanamke ambaye amekubali kuolewa sharti ajue majukumu yake katika ndoa. Umekubali kuwa mke wa mtu wew ni mama wa familia na majukumu yote ya kumuhudumia mumewe pamoja na familia watakayoiunda. Chamsingi asisahau agano lake kwamba mwanamke na amtii mumewe.
👉Mwanaume ambaye amekubali kuoa bila kulazimishwa lazima akubaliane na hili kwamba ndoa ni majukumu, hvyo hvyo pia uanaume ni majukumu. Mume ni baba wa familia, na uwe tayari kuitunza familia mtakayoiunda mahitaji yote ya familia sharti baba atimize, mwanaume umekubali kuoa mwanamke uliyempenda basi jiapie kuishi na mwanamke huyo Huyo ulieona ni sahihi kwako. Chamsingi asisahau agano lake kwamba mwanaume na ampende mkewe.
Basi mweenyenz mungu awajalie ndoa zenye maelewano, mafanikio, upondo na amani ili muweze kufikia kweny malengo yenu. Asiwepo yeyote wa kuvunja agano Lenu.
Like
Share
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU