Dada zangu:
Mwanaume yeyote aliyekuacha kwa dharau, dhihaka, matusi au hata kukuonyesha uchafu aliokuwa akiufanya na wanawake wengine, akiomba mrudiane naye usikubali.
Mwanaume yeyote aliyekuacha kwa dharau, dhihaka, matusi au hata kukuonyesha uchafu aliokuwa akiufanya na wanawake wengine, akiomba mrudiane naye usikubali.
Nakusisitiza tena, USIKUBALI. Kama alishindwa kutambua thamani yako wakati mpo pamoja hadi mkaachana, hawezi kuitambua tthamani yako mkirudiana. Furaha ya mwanaume kama huyo ni kumuona mwanamke aliyeachana naye akipata shida, akilia na kuuzunika katika maisha yake.
Mwanaume hujihisi fala pale anapokuona unaendelea na maisha yako kama kawaida, unafuraha na amani katika moyo wako, humtegemei wala kumlilia kama ulivyokuwa ukilia hapi awali juu yake, hivyo atafanya kila liwezekanalo mrudiane then akurudishe kwenye vikwazo ulivyovivuka.
Endelea kumuomba Mungu akupe ujasiri wa kusimama mwenyewe katika maisha yako. Muombe sana Mungu aendelee kuyalinda mahusiano yako mapya, ampe imani ya kukujali huyo mwenza wako mpya, akupende na kuyafanya mahusiano yenu kuwa yenye tija.
Muepuke sana mwanaume aliyekuacha kwa mbwembwe kisha anarudi kwa hekima akitaka mrudiane baada ya kukuona umefanikiwa kuyashinda majaribu yake na furaha yako kuimarika.
Like
Share
Like
Share