Moja ya sifa kubwa ambayo itamfanya mke/mpenzi wako kukupenda na kufurahia kuwa na wewe ni kujiamini. Wanawake pamoja na kupenda pesa sana, pamoja na kupenda shughuli nzito Kitandani lakini kama hujiamini basi utamboa kirahisi mke/mpenzi wako na utamlazimisha kama si kuchepuka basi kukuacha na kutafuta mwingine.
Kujiamini kwa mwanaume haimaanishi sijui kuwa na mijinguvu na kupigana au hata kumpiga, haimaanishi kumnyanyasa na kumtolea maneno ya kashfa, haimaanishi kutokumjali au kujali mambo anayoyafanya. Hapana, inaanisha kwanza kujikubali wewe mwenyewe, kwamba pamoja na kasoro zote ambazo unazo kama binadamu lakini unajikubali.
Unakubali ulivyo na hujilinganishi na wanaume wengine, hujilinganishi na Bosi wake, hujilinganishi na jirani yenu, hujilinganishi na Kaka yake, hujilinganishi na mume wa shoga yake. Hapana unajiamini kua umeshampata yule mwanamke, kwamba unampenda na mpaka kukubali basi kuna kitu nayeye amekipenda kwako.
Punguza wivu, hapa sisemi usiwe na wivu na ukubali mambo ya kifala hapana, lakini uwe wa kipimo, wanawake hupenda wanapoonewa wivu lakini ukizidi unakera. Kwamba kama wewe ni yule mwanaume ambaye kila siku ni kukagua simu ya mke/mpenzi wako, kama wewe ni yule mwanaume wa kupaniki na kugombana ukimuona tu kasimama na mwanaume mwingine.
Kama wewe ni yule mwanaume wa kumchunga hutaki atoke, hutaki afanye hata kazi kisa unaona utaibiwa. Ndugu yangu kwanza unapaswa kufahamu kuwa unamkera mke/mpenzi wako, pili nikama unamuambia kuwa hujiamini una wasiwasi na uanaume wako na tatu atachoka na nina uhakika kama si leo basi kesho atakusaliti tu kwani hana furaha hivyo akipata mtu anayejiamini atakuacha unang’aang’aa macho.