-->

KUNA TOFAUTI KATI YA KUTESWA KWENYE MAHUSIANO NA KUJITESA KWENYE MAHUSIANO!


(1) Hujawahi kumfumania mwenza wako lakini kila siku una kazi ya kukagua simu yake ili kutafuta kama anachepuka au la! Hukuti kitu lakini kesho yake bado unahangaika basi wewe jua tu unajitasa kwenye mahusiano na kama una hii tabia jua tu kuwa hata ukimfumania, narudia hata ukimfumania hapo anafanya huwezi kumuacha! Yaani kama wewe ni mtu wa kukagua simu kutwa mara tatu, awe ni mume, mke, mpenzi au nani basi huna ujasiri wa kumuacha, ni sawa na Mbwa kukimbiza gari, hainamaana anajichichosha tu kwani hata akilikamata hawezi kuliendesha hivyo acha kujichosha.
(2) Kumfuatilia kila mtu anayeongea na mpenzi wako; Unayafanya mahusiano yako au ndoa yako kuwa kama mahakama, kwamba mwenza wako kila dakika anatakiw akujielezea kwako, anaongea na mfanyakazi mwenzake basi anatembea naye,k kuna mtu kamsalimia labda wewe kakupita basi anatembea naye, kuna mtu kamchekea basi unauliza ni nani na anatembea naye! aina hii ya mahusiano inaboa na mara nyingi mtu akichoka unakuta ushaachwa bila kujijua kwani mtu anajiona kama yuko mahakamani anatakiwa tu kujitetea kila dakika!
(3) Wale watu ambao kila kitu wanahisi wanadharauliwa; Hawa ndiyo wanajichosha na kujinyanyasa mpaka basi, mtu kachelewa kupokea simu ushaanza ananidharau kwakua sina kazi,a nadharau kwakua kwao wanapesa, anadharau kwakua hivi vile, yaani mtu kashaaua kitu ulichomuambia jana yake unahisi unadharaulika, mtu kakose akidogo unahisi nikwakau kakudharaau, simu imekatika bahati mbaya au amekuambia yuko bize, hajajibu meseji yako wewe ni kudharaulika mpaka basio, unalazimisha udharaulike, ukijiona hivi basi jua kuwa hunyanyaswi bali unajinyanyasa!
Kama una tabia hizi za kujitesa basi jua kuwa mwenza wako hata akupe dunia bado hutaamini, hicho uanchokilalamikia kila siku akikupa utatafuta kingine. Inawezekana kweli mwenza wako ni msheniz lakini kinachjokuumiza si ushenzi wake bali kwakua huna amani ya nafsi. Amua leo, najua ngumu lakini amua kubadilika, hembu sema kuwa sitaki kitu flani naacha kitu flani. Utaona kuwa unabadilika unakua na furaha na mwenza wako naye anakufurahia. Jifunze namna ya kujipa furaha yako mwenyewe, soma kitabu cha “ndoa Yangu Furaha Yangu” Se4hemu ya nne, naa cha kujitesa mwenyewe huku ukisingizia unateswa.
idd makengo
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU