-->
Showing posts with label KUTONGOZA. Show all posts
Showing posts with label KUTONGOZA. Show all posts

Kuna mambo katika usichana wako ...katika usingle wako usiwe nayo mpaka yakapitiliza .

.maana yakipitiliza hautaonekana tena kama ndani yako kuna ustaharabu.
Mambo hayo ni pamoja na:
KURINGA KUPITILIZA.
Hakuna anaekukataza kuringa ..By the way wewe ni mwanamke ringa .. LAKINI KURINGA KWAKO KUSIPITILIZE.. Utamkwaza hata yule aliye na nia njema kwako...hataona tena kuringa kwako bali ataona bado kuna utoto ndani yako..
Ataona bado haujawa tayari kuwa mwanamke.
Sijajua kwa sisi wanaume kama kuna alieoko hivi...Kama yupo mwanaume anaringa namna hii basi aundiwe tume ya uchunguzi ...maana sio bure... Kutakuwa na mkono wa mtu...
KUWA NA KIBURI KISICHOKUWA NA MBELE WALA NYUMA.
Hii imewakosesha wasichana wengi watu waliokuwa na nia njema kwao na kujikuta wameangukia kwenye mikono mibaya ..mikono ya watu wanaokuona unakiburi lakini hata hawaangaiki na wewe maana wanajua wanapita hapo... wamepuzika kunywa maji ..then safari yao iendelee.
KUPENDA STAREHE KUPITA KIASI:
Hizi starehe za pombe na nyama ..kwamba usipozipata haujisikii poa ...uko tayari uuze utu wako lakini upate pombe nyama..
Hii ni mbaya sana kwako mwanamke ..maana mwanamke wa namna hii mara nyingi huangukia mikono ya wajanja ..hakuna mwanaume anaejielewa aje akuvamie ...wewe utakuwa unavamiwa na watu wa kukutoa out then ndani ya muda mfupi wanatembea na wewe kisha wanakuacha... Kumbuka kila mtu anapenda starehe ila isipitilize maana ikipitiliza saba itakufanya wanaume wakudharau.
Dayari Yangu
Image may contain: 1 person, standing, child, hat and outdoor
Share:

Haya ndio Mambo Huwafanya Wanawake Wengi Kushindwa Kuingia Katika Ndoa (Kuolewa)


Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.

Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)

Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.

Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi. Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari. Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.

Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.  Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kuna wanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa. Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati.  Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.

Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa
Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka. Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo. Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa. Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.

Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani. Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamo wake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana. Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.

Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa. Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi. Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa. Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa. Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.

Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume -  Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto.  Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.

Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia. Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.  Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.

Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa.

Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi. Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.  Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
Share:

Njia Nne Za Kufanya Ili Uongeze Kujiamini Kwako kwa Wanawake sanaa ya kutongoza, wanaume

NJIA ZA KUTONGOZA – Page 3 – My Blog
Kuweza kujiamini kwa mwamume ni jambo muhimu katika huu ulimwengu ambapo kunatofautisha kati ya mwanamume thabiti na wale feki. Kila mwanamume anajaribu kuimarisha kujiamini kwake katika huu ulimwengu. Lakini ushawahi kujiuliza ni mbinu gani unazofaa kutumia ili uongeze ama kuimarisha kujiamini kwako? Wengi wasiojua mbinu za kutumia kuwa na confidence wanabakiwa na kutumia mbinu ambazo mwishowe zinawaweka katika hali ambayo inakuwa aibu kwao.
Tukiongea kuhusu maswala ya kujiamini, wanaume wengi kujiamini kwao mara nyingi hutumika wakati ambapo anajaribu kumtongoza mwanamke fulani ama wakati ambapo anajaribu kumridhisha mpenzi wake ili azidi kumpenda zaidi na zaidi.
Well, kwa wanaume, kuna wale ambao wanajiamini na kuna wale ambao bado kujiamini ama kuwa na confidence kwa mwanamke ni tatizo.Labda kuna mwanamke ambaye ushawahi kujaribu kumtongoza halafu baada ya siku ama madakila ya kuongea naye anakupuuza ama anakudhalilisha mbele ya marafiki zako. Usikate tamaa kwani bado una nafasi kubwa ya kujua kosa lako limetokea na wapi.
1. Jikumbushe kuwa wewe ndiwe wewe
Wanaume wengi wanafanya makosa makuu ya kujidhalilisha kibinafsi. Hii inatokea pale ambapo mwanamume anapomakinika na mambo ambayo yanamfanya yeye duni. Maneno ya kujiona kama wewe hufai ama kujiona kuwa mwanamke unayemfukizia hatapendezwa na tabia zako unafaa kuyatupilia mbali. Unafaa kumakinika na mambo ambayo yana uzuri kwako. Mfano kujiamini ya kuwa una kipawa cha kuongea, kuchekesha nk. Kujiamini huku kutamfanya mwanamke kukudhanimi. So kazi ni kwako, aidha usijiamini mwanamke akudharau ama ujiamini wanawake wakuandame kama vile kivuli.
2. Usimakinike sana na urembo
Kosa jingine ambalo wanaume wengi wanafanya ni kuwa wanamakinika sana na urembo wa mwanamke. Ukweli usemwe, ukiwa umezungukwa na wanawake wengi warembo kwa kawaida inakuwa vigumu kumakinika na yale ambayo unasema. Hii hutokea kwa sababu ya kufikiria sana urembo wa mwanamke kiasi ya kuwa unapunguza kujiamini kwako. Kusuluhisha hili tatizo hakikisha ya kwamba wakati ambapo unapokuwa na mwanamke mrembo yeyote, weka kwa akili yako kuwa mwanamke huyu ni mbovu na hana lolote na urembo, hii itakupa wewe uwezo wa kumwona mwanamke unayeongea naye ni wa kawaida hivyo kukupatia nafasi rahisi ya kuongea naye bila tatizo.
3. Shughulika na maswala mbadala
Wakati mwingi ambapo mwanamume anapokuwa date na mpenzi wake ama kukutana na mwanamke kwa mara ya kwanza, kitu ambacho anakiweka mbele ni malengo na madhumuni ya kutaka kitu kutoka kwa mwanamke. Aidha inawezakuwa anataka namba ya simu, kupewa date nyingine ama kitu tofauti mbali na haya.
Ok mbona usimakinike utulie uje na mtindo mpya ambao utakufanya uwe na confidence kwa mwanamke yeyote? Jaribu kuleta maswala ambayo hayalengi ajenda yako kwa mwanamke ili uweze kupata confidence. Njia hii inapunguza wasiwasi wako ambao unaweza kuwa nao kwa mwanamke yeyote. Mwishowe wakati umemzoea itakuwa rahisi kwako kuweza kumwambia chochote ambacho umekuwa ukitaka kumwambia.
4. Rudiarudia
Wataalamu wengine wangepinga mbinu hii ya kutumia kwa mwanamke wakati wa maongezi lakini kwa mtizamo flani hii ni njia muruwa ya kutumia wakati wa kujenga kujiamini kwako kwa mwanamke. Kama una mistari ambayo umeishika na kwa kawaida unaitumia wakati unapokuwa na mwanamke na umeshuhudia kuwa inafanya kazi kila wakati, mbona usiitumie tena na tena kwa mwanamke unayemzimia kwa sasa? Hii kando na kukupatia confidence, itakupa nafasi ya kuonekana mtulivu na kukuona kama unajua kupanga maneno yake vile inavyotakikana.
Kujifunza kujenga kujiamini kwako kando na kuwa kutakuwezesha kuweza kuongea na wanawake kwa urahisi, pia kutakuwezesha wewe mbeleni kuweza kukabiliana na mambo kadhaa na kufanikiwa maishani.
Share:

FANYA HIVI UNAPOVUTIWA KIMAPENZI NA MTU MWINGINE TOFAUTI NA YULE ULIYENAYE KWA SASA

Ufanye nini unapovutiwa kimapenzi na mtu mwingine


Wapo watu ambao wameoa au wana wapenzi walioahidiana kwa mambo mengi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kuvutwa kimahaba na watu wengine. Hali hii huwatokea wawapo masomoni, kazini, kwenye biashara, mbali au pengine hata karibu na wenza wao wa zamani.
Sayansi ya jamii inakubali kuwa mwingiliano wa kijamii mara nyingine huathiri tabia za watu, ukweli huu unathibitishwa na ongezeko la usaliti katika mapenzi, mantiki ikibaki kwenye mwili kulazimishwa na mapokeo ya tafsiri ya vitu vinayotawala mawazo ya mwanadamu.
Katika mapenzi kuna mashujaa wachache sana ambao wanamudu ushawihi wa kimahaba kutoka kwa wengine, hii ina maana asilimia 96.5 kwa mujibu wa uchunguzi huanguka kwenye mapenzi mapya baada ya miili kuelemewa na hisia chochezi.
Maelfu ya wanaume na wanawake hulazimika kuwasaliti wapenzi wao baada ya kuvutiwa na maumbo au sura za wanaume/wanawake wanaokutana nao katika shughuli zao za kimaisha. Wapenzi hao hujikwaa kupitia macho na hisia zao, huku wengi wakikiri kushindwa kuzuia matamanio.
“Msichana/mvulana huyu ni mzuri sana nahisi kumpenda, nimuonapo nachanganyiwa kabisa.” Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya umewahi kutamka maneno haya na ukasahau kuwa umeoa/ umeolewa au una mchumba uliyepanga kufunga naye ndoa.
Kama hilo halitoshi yawezekana umeshakuza mawazo hayo kiasi cha kuona huna jinsi zaidi ya kufanya usaliti, ukatongoza au ukajitongozesha kwa gharama ili utii hisia zako.
Ninapotazama mwenendo wa wapenzi wengi siku hizi, nabaini kuwa mihemko ya miili inawaangusha wengi kwenye usaliti, jambo linalonifanya nilazimike kufundisha namna ya kukabiliana na tatizo hili ili kuweza kuyanusuru mapenzi .
Naliita jambo hili tatizo kwa sababu limeleta madhara mengi katika jamii, kuna watu wameshauana, ndoa kusambaratika na mapenzi kufa, isitoshe uchunguzi unaonyesha kwamba, wasaliti wengi hawakupata faida au raha waliyoitarajia kutoka kwa wale waliowashawashi, hivyo kufanya hisia zao ziwe kazi bure.
Naamini hakuna mwenye akili timamu anayependa kupoteza utu wake bila faida. Ndiyo maana ipo orodha ndefu ya watu walionifuata na kukiri: “Alinirubuni nikamwacha mpenzi wangu, kumbe alitaka kunichezea tu.”
Wanakiri kurubuniwa, lakini wanasahau kuwa walikubali baada ya kuvutwa na hisia! Je mpaka sasa ni wanaume wangapi wanavutwa kimahaba na akidada warembo wanaokutana nao kiasi cha kuwapuuza wapenzi wao wa zamani na kuamua kuwasaliti?
Katika matembezi yao, shughuli zao, ni wasichana wangapi wanachanganywa na muonekano wa wavulana wanaofanya nao kazi. Angalia mwenendo wako utabaini umekuwa kwenye mtego huu mara ngapi.
Je umeshawahi kujiuliza: HUYO UNAYEVUTIWA NAYE ATAKUCHUKULIAJE? Unachofikiri ndicho anachofikiri yeye au unajipendekeza? Jaribu kuwaza kama unajipendekeza hatma yake itakuwaje kama si kupoteza utu wako bure.
Jiulize tena, UTAPATA NINI KWAKE. Watu makini hujiuliza faida watakazopata katika matendo yao na hivyo kuwa na maamuzi sahihi. Kukurupuka kufanya jambo bila kutazama faida na hasara zake ni wendawazimu. Swali jingine, UNAYEMBABAIKIA ATAPATA NINI KWAKO, Je asipopata cha maana ataamuaje?
Baada ya kujiuliza hivyo, malizia kwa kujiuliza UKO SAHIHI? Kitalaamu ukitoa nafasi ya mawazo yako kuhakiki mienendo yako, utajikuta mwili wako haukulazimishi sana kutimiza matakwa yake, lakini ukiwa mtu mwenye kuona na kulea hisia, utajikuta siku moja unafanya jambo baya litakalokuumiza maisha yako yote.
Waendekezao hisia za mvuto ndiyo hao wanaodiliki kufanya mapenzi hata na baba, mama, kaka na dada zao.
Share:

MWANAMKE JIFUNZE KUMFAHAMU MWANAUME ANAYEFAA KUWA MPENZI WAKO KABLA HATA HAJAKUTONGOZA.


Wanaume ni wengi ambao watakuapproach. Wengine ni wazuri umependezwa nao na wengine hujapendezwa wao. Lakini je, utajuaje ni mwanaume yupi anayefaa katika maisha yako? Kuna wanawake wengi ambao wamekabiliwa na mateso ya kuachwa na mwanaume mmoja hadi mwingine kisa ni kuwa hawajui kuchagua. Si kila mwanaume anayekuappoach na kukutongoza unapaswa kumkubali. Kile kinachohitajika kwanza ni kuhakikisha kuwa unamsoma na kuzijua tabia zake kabla hujaamua kumkubali.
Hapa Dakari Mapenzi tumekuja na vigezo vya kuangalia na kuchunguza kabla ya kumchagua mwanaume.
 Zama nasi...
#1 Huwa anapanga mambo na wewe.  Ukimwona mwanaume ambaye anakuhusisha katika maamuzi yake basi fahamu hapo ndipo. Mwanaume ambaye atakuambia na mapema kuhusu mambo anayoyapanga wikendi ya kutoka pamoja basi jua huyu ni mwanaume ambaye anaonyesha dalili za mwanaume bora.
#2 Anakumbuka mambo masuala ambayo uliyazungumza kitambo na kuyaleta katika mazungumzo yenu. Hapa sio siri. Kila mwanamke anapenda mwanaume ambaye anakumbuka mambo ambayo alimwambia ama alimfanyia kitambo. Mfano mwanamke husisimka haswa wakati ambapo mwanaume anamwambia jinsi mara ya kwanza walipokutana na jinsi alivyovalia. Hii ni ishara dhabiti ya kuonyesha mwanaume kama huyu anakudhamini. Ukimwona mwanaume ambaye hakumbuki hata jina lako basi huyo mueke mbali sana.
#3 Haangalii picha zako fb/instagram pekee bali pia ana comment. Kama unazungumza na yeye kwa comments zako bila tatizo basi huyu hata mnaweza kuoana naye hapo hapo :)
#4 Kukutumia na kujibu text zako si tatizo. Ukiona mwanaume anachukua karne nzima kabla kukujibu text yako basi hapo atakuwa labda anawengine anaowaweka umuhimu zaidi kukuliko. Lakini ukimwona anamakinika na wewe katika kila jumbe basi hapo ndipo, usichelewe.
#5 Yuko serious na maisha yake ya mbeleni. Mwanaume ambaye anayapanga maisha yake ya mbeleni ni mwanaume bora kati ya wote. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa mbeleni hataki kupitia mateso yeyote wakati ambapo atakuwa na kipenzi chake ubavuni mwake. Hivyo wewe unapaswa kuchukua jukumu la kuhakikisha kuwa unayafanikisha maisha yake ya usoni kwa kuwa naye.
#6 Hajali iwapo anaonekana mshamba akiwa anadensi. Utafiti unaonyesha kuwa wanaume ambao hawajui kudensi karibu mara zote huwa ndio wanakuwa boyfriend bora zaidi.
#7 Anampenda mamake na yule mama mboga. Iwapo mtu anawapenda wanawake ambao waliyafanikisha maisha yake na pia wale ambao waliyafanya maisha yake kuwa rahisi, basi pia kwako atakuwa mzuri. Hili ni jambo ambalo limefanyiwa uchunguzi wa  kina.
#8 Anapenda wanyama. Ok ni kusema tu, kuna kitu flani ambacho kinajitokeza wakati unapomwangalia mwanaume mkubwa akimbabaikia paka mdogo ambaye analia. “NI LAZIMA UMDETI MWANAUME AINA HII HARAKA SANA.”
#9 Anakufanya ucheke. Kila mwanaume atafanya juu chini ucheke. Hivyo iwapo unamwona mwanaume anajikakamua ucheke usijilazimishe. Hakikisha kicheko chako kinatoka naturally kwa mambo ambayo yanakufanya ucheke. Anyway, ukimwona  mwanaume anakupendeza na vicheko vyake basi ni ishara ya kuwa ni mbora.
#10 Nyote wawili mnazimia kipindi kimoja cha runinga. Hii ni ishara ya kuwa nyote wawili mko na interest inayofanana, so mkiungana kuwa kitu kimoja pia si vibaya.
#11 Haongea ubaya kuhusu mpenzi wake wa zamani. Mwanaume ambaye anatabia za ujentleman basi haitawahi kutokea hata siku moja ambapo atamtukana ama kumkejeli mpenzi wake wa zamani. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii achana naye mara moja coz pia wewe atakufanyia vivyo hivyo.
#12 Anawaheshimu wanawake. Mwanaume anayewaheshimu wanawake bila shaka naye atakuheshimu. Hivyo basi usitupe mbao wala kumkataa mwanaume aina kama hii, ni wachache sana hapa duniani. 
Hivi ni baadhi ya mambo ambayo ni dalili ya kuonyesha kuwa mwanaume flani anafaa kuwa boyfriend wako.  Na si lazima aonyeshe ishara hizi zote ndio umwone anakufaa, la. Iwapo ataonyesha baadhi ya ishara hizi basi usingojee mpaka apoteze tamaa kutoka kwako.
Share:

Mwanaume Anahitaji Vitu Hivi Tu Ili Kudumu na Mwanamke Kwenye Mahusiano


Wanawake wengi hufanya kila aina ishara ya upendo kwa wanaume zao, lakini cha ajabu wanaume hao bado hutoka nje ya ndoa zao na kwenda kutafuta vimada, kitu ambacho wanaweke hukosea ni kwamba wanawake hao huonesha upendo kwa wanaume zao, lakini ukweli ni kwamba asilimia tisini na tisa( 99%) ya wanaume dunia kote hawahitaji upendo kutoka kwa wapenzi wao, bali mwanaume yeyote yule anahitaji kitu hiki ili mdumu katika mahusiano ya ndoa:
1. Mwanaume huhitaji heshima kutoka kwa mpenzi wake.
Kitu kikubwa ambacho mwanaume anakihitaji kutoka kwa mpenzi wake ni heshima, na si upendo kama wengi wazaniavyo, mwanaume yeyote yule akioneshwa heshima kutoka kwa mwanamke wake huisi kupendwa zaidi. Hivi hushangai kwanini wanaume wengi hutembea na wafanyakazi wao wa ndani?
Unadhani wafanyakazi wa ndani wanajua kupenda zaidi? La hasha wafanyakazi wandani hawajui kupenda kwa asilimia mia moja ila kinachowabeba ni kule kuwa heshima, na heshima hiyo ndiyo inamfanya wanaume wengi kutoka kimapenzi na wafanyakazi hao.
Hivyo ewe mwanamke mpenda kudumu katika mahusiano ya kimapezi, ongeza heshima kwa mwanaume wako kadri uwezavyo, kwani mwanaume wako anahitaji heshima na si upendo kama we uzaniavyo.
2. Mwanaume anahitaji umuamini.
Japo jingine ambalo mwanaume wako anahitaji kutoka kwako ni vile ambavyo unamuamini, kujenga imani na mpenzi wako ndiyo siri kubwa sana ya kudumu katika mahusiano yenu.
Kutokujenga imani na mwezi wako ni mwanzo wa kubomoa mahusiano yenu, hivyo kama itakuwa ni ngumu kujenga imani hiyo unachotakiwa kufanya pale mambo yakiwa hayaendi sawa ni heri kumwambia kuliko kukaa kimya.
Hayo ni mambo ya msingi ambayo unatakiwa kufanya ili kudumisha mahisiano yenu yaweze kwenda mbele daima.
Share:

NENO NAKUPENDA NI RAHISI KUSIKIKA INAPOTAMKWA,TAMU MASIKIONI LAKINI ISIPOENDANA NA VITENDO HALISI HUWA CHUNGU KAMA SHUBIRI MOYONI.


Kama mtu anakupenda na anakujali lazima atafanya jitihada ya kutengeneza muda wa kuwa karibu na wewe bila ya kujali ubize au umbali uliopo baina yenu.
Atakuwa karibu na wewe kwa kila namna, atajivunia kuwa na wewe na ataonesha wazi namna anavyofurahia uwepo wako kwake.
Hivyo, kuwa makini. Usihadaiwe na hizo Nakupenda sana au nimekumiss sana. Lazima kuwepo na jitihada za kumaanisha maneno hayo.
Kumbuka, muda ni mali adhimu, usikubali kuchezewa michezo ya kitoto ukapoteza muda wako. Okoa moyo wako na muda wako kwa watu wasio serious na mahusiano yasiyokujenga zaidi ya kuzidi kukumaliza kiuchumi na kifikra.
Share:

Wanaume Hutongoza Wanawake Wanaowaona; Hii ndiyo sababu ya kwanza ya mwanaume kumtongoza mwanamke.

Wanaume Hutongoza Wanawake Wanaowaona; Hii ndiyo sababu ya kwanza ya mwanaume kumtongoza mwanamke, kwamba ili wewe mwanamke uitwe na mwanaume akuombe namba yako ya simu na kukutongoza, nilazima huyo mwanaume akuone kwanza, kwamba hata kama umzuri kama Malaika kama unajifungia ndani basi hutapata mtu wa kukutongoza hivyo hutapata mume!
Labda nifafanue kidogo, hembu angalia ratiba yako wewe mpweke, unaamka asubuhi, unajiandaa unaenda kazini, huko unakua bize na kazi na unaonana na wafanyakazi wenzako ambao washakuzoea waaala huataki na wao hawakutaki! Ukitoka ni kwenye daladala nyumbani, huko unakaa weekend wewe ni kujifungia ndani.
Sasa watu unaokutana nao ni wafanyakazi wenzako ambao tayari mshazoeana nao na hawakutaki, kwenye dadala kuna watu na stress zao hata hawakuoni, kama una gari ndiyo hata hukutani na mtu! Majirani zako ambao nao wote wameoa au tabia zao ushawachukia! Sasa Dada yangu ukimuomba Mungu akupe mume unataka muoneshe hapo chumbani!
Au unataka utongozwe na Kabati ambalo unashinda nalo kila siku? Ili mwanaume kutongoze nilazima akuone, ukitaka mwanaume mwenye hela nenda sehemu wanapokaa wenye hela, ukitaka mfanyabiashara hivyohivyo, acha kujifungia ndani ukidhani ni tabia nzuri, ukidhani ndiyo wanaume watakutongoza. Kwakua umetulia ukitoka kazini ni nyumbani, umetulia kweli lakini hawakuoni!
Umzuri lakini huwezi kujitongoza mwenyewe, hembu toka na marafiki, hudhuria matukio, toka mwenyewe, nenda sehemu za starehe. Sisemi uwe mtu wa bata hapana lakini nasema utoketoke hata nnje wanaume wakuone wakutongoze, hawawezi kukuonea huko ndani kwako. Tafuta sehemu za kistaraabu nenda utakutana na wastaarabu wenzako watakutongoza na kukuoa!
Share:

JE UNATAFUTA MCHUMBA AU MPENZI KWENYE MTANDAO?? NGOJA NIKUPE SIRI HII ITAKUSAIDIA.

Iddi Makengo - UMEKUA MPWEKE NA UNATAMANI KUTONGOZWA ILI... | Facebook
Kumtafuta mwandani wa moyo wako kwenye mtandao ni jambo la kuvutia sana; japokuwa kuna umuhimu wa kupata hatari. Kwasababu tayari una aina nyingi ya watu, lakini pia huna uzoefu wa kukutana na jamii kubwa ya watu na unawakati mgumu kupambanua ni mtu yupi anakidhi vigezo vya mtu unayemtafuta. Sasa yapo mambo ya kuzingatia katika matazamio yako ya kumtafuta mchumba wako ndani ya mtandao. Hivi vitu adimu ambavyo naenda kukupa vitakusaidia kukuweka mbali na mwanaume au mwanamke ambaye siye unaye mtafuta.
Jambo la 1.
Anza taratibu. TAMBUA HII kuwa kuna aina ya yote ya watu katika himaya ya mapenzi; na siyo watu hawa wote watakufaa. Chukua muda wako –kama umekutana na mtu kwa mara ya kwanza na anza mazungumuzo ama kuchati naye taratibu na kumgundua kama ndiye. Mtu huweza kujisifu kuwa yeye yuko hivi ni mpaka wewe umgundue hivyo na sisitiza kuwa chukua muda wako kumchunguza kwa makini tabia yake ya mwazo na ya sasa. KAMA KUNA KITU kimekutatiza ni RAHISI TU achana naye. Chukua virago vyako. KAMWE USIKIMBILIE MAHUSIANO YOYOTE YA KIMAPENZI KABLA YA KUFIKIRIA KWANZA.
Jambo la 2.
Linda Utambulisho wako (protect your Identity). Moja ya faida ya kumatafuta umpendaye kwenye matandao ni kwamba utajikuta unamjua mtu haswa kulingana na haiba yake. Inabaki kuwa uamuzi wako kuwa ni wakati gani kujionyesha kuwa wewe ni nani haswa lakini yakupasa kuwa makini sana, Ingawa pale mtu anapopokea haiba (personality) anaweza kuitumia kinyume na matwakwa yako. Kama mwenzako anakupa presha juu ya wewe kumpa jina lako la mwisho, email yako, anwani ya nyumbani kwako, namba ya simu, na mahala ambapo unafanyia kazi na vitu vinginevinavyokutambulisha wewe…ACHANA NA HUYO MTU.
Jambo la 3.
Tumia Akili. Wakati unapozungumza na mtu kupitia himaya ya Mapenzi, usitupe maamuzi mazuri mbali eti kisa hii ni huduma ya kimtandao. Jambo ambalo linaweza sikika vizuri na likahamasisha ni kuwa umempata mtu ambaye umemjua vizuri. Kuwa na tahadhari na uzitumie hizo tahadhari, na USIANGUKE katika kumpenda mtu eti kwasababu umevutiwa na wasifu wake uliousoma kwenye mtandao. Chukua muda wako pia pitia kila maeneo muhimu.ya chaguo zako. Baada ya kufanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha vya kutosha. Ni mazoea sana watu huanguka katika mapenzi baada ya mazunguzo ya kwanza. USIRUHUSU HILI. Jitahidi kudumisha akili yako na kuona kuwa kumtafuta umpendaye kwenye mtandao ni sawa na utafutaji wa mchumba ndani ya dunia yetu hii ya kawaida. Haipaswi kupenda kila wasifu unaousoma.
Jambo la 4.
Omba Picha. Unapokutana na mtu, chati naye, na ona jinsi mwanzo wa mahusiano unavyokuwa unajengwa hapo itakupeleka kuona kuwa unaweza ukaomba picha. Hii itakupelekea hasa kukupa taarifa zaidi kuhusu mtu mwenyewe kuliko email na chating zingine zinazofanyika. Awali ya yote itaondoa uongo wa kila mtu anavyomtazamia mwenziye kuwa yukoje. Utajua pia anakuvutia kimuonekano? Ama La! Mwisho kama anashindwa kutuma picha yake, huenda kukawa na sababu. NENDA KWA UANGALIFU
Jambo la 5.
Kuwa Makini. Hili linawezekana, ni jambo la muhimu sana ukilifuata. Katika email, kila mtu anaweza kusikika vizuri lakini katika uhalisia si yeye .mnapokuwa umejiingiza katika himaya ya uchumba ama mapenzi na mtu pia tegemea bendera nyekundu ama tabia za zamani. Pia weka umakini katika majaribio yoyote ya kukupa presha ama kukutawala. Mwisho angalia sana na kuwa makini na taarifa zile ambazo mchumba wako anakupatia ama majibu ya maswali unayomuuliza. Kama uhusiano wako unaonyesha mambo yafuatayo. Unashauriwa kuangalia upya mahusiano yako;
1. Kama mwanamke/ mwanaume hatoi majibu ya kweli kuhusu umri wake, vitu anavyopendelea, mwonekano, taaluma yake na ajira yake.
2. Kama anakataa kuongea na wewe kwenye simu baada ya kuanzisha mahusiano ya kwenye mtandao.
3. Kama hatoweza kujibu kwa ufasaha maswali mtakayokuwa mnaulizana. Je atakuwa anakujibu maswali vizuri ama anakurudishia swali kwako.
4. Kama atakupa picha ya kikundi cha watu waliyopiga pamoja na yeye akiwemo itakayofanya kuwa vigumu kumtafuta. Kutafuta mchumba mzuri umpendaye kwenye mtandao ni jambo zuri na linahamasisha na linatimiza ndoto zako. Wewe kumbuka tu kufuata mambo muhimu hapo juu na fanya kama yanavyoelekeza na utafanikiwa.
Share:

JINSI YA KUMPATA DEMU ANAEONEKANA MGUMU KUPATIKANA

JOHARI - Mwananchi
#MWANAMUME yeyote anapotaka kumtongoza mwanamke hulazimika kwanza kumwonesha – japo kwa matendo – kuwa anampenda, au kwamba amevutiwa naye. Hatua hii ndiyo yenye changamoto kubwa zaidi kwa mwanamume, maana ndipo wakati anapokuwa anajaribu kufikisha hisia zake kwa mkusudiwa huku yeye mwenyewe akijihakikishia kuwa ndio anatengeneza.
Mwanamume anapokuwa anajaribu kuzifikisha hisia zake za kimapenzi kwa mwanamke, mapigo ya moyo yanaweza kumwenda mbio kama amekutana na jini, hususan kama mwanamke anaonekana kuwa “maji Makubwa”. Hata hivyo, ni kazi ambayo kila mwanamume hulazimika kuifanya.
Kazi hii ya kuelezea hisia zako kwa mwanamke, tena kwa mara ya kwanza huhitaji umakini na ujasiri wa hali ya juu zaidi. Bahati njema, shughuli yenyewe ina sayansi yake, ambayo ina misingi katika mahusiano ya kijamii. Ukifahamu sayansi hii inaweza kuwa rahisi zaidi kwako kwa kufikisha hisia zako kwa mlengwa – na kufanikiwa (100%).
1. KUKUTANISHA MACHO NI MUHIMU
Kawaida, mambo yote huanzia – na pengine kuishia – katika kukutanisha macho. Mwanamke atakapobaini kuwa hujajaribu kumwangalia japo kwa sekunde mbili mfululizo, ataondoa mawazo na hisia zake kwako hata kabla hujasema neno lolote.
Macho ndizo zana muhimu zaidi mtu anapokuwa anataka kuonesha hisia kwa mwenzake kuwa anampenda, au amevutiwa naye. Hii ni kwa sababu macho ndiyo vipitisho na visambazaji muhimu vya ishara baina ya mtu na mtu, hata kama si katika masuala yanayohusiana na mapenzi.
Kukutanisha macho na mtu wa jinsia nyingine unayevutiwa naye au anayevutiwa nawe ni jambo lenye nguvu za ajabu katika kuanzisha uhusiano. Kwa sababu hiyo, hata unapofanikiwa kumtazama moja kwa moja machoni mwenzako hutarajiwi kutumia zaidi ya sekunde mbili, kutokana na nguvu iliyomo katika mawasiliano haya.
Katika hili, wanaume mahiri hufahamu ni wakati gani wa kumwangalia mwanamke na ni wakati gani wa kutomwangalia. Mara nyingi, ni vizuri zaidi kumwangalia zaidi mwanamke wakati anapozungumza, huku ukikwepesha macho kidogo pale unapozungumza wewe.
2. UNATAKIWA UWIANO, UKWELI KATIKA MAZUNGUMZO
Ni jambo lisilopingika kwamba wanaume na wanawake wanatofautiana katika maana na dhana ya mawasiliano. Hata hivyo, bado inawezekana kuendesha mazungumzo shirikishi na yenye kuburudisha ukiwa na mwanamke, bila kuonekana wa bandia.
Watu wa jinsia zote mbili wanaweza kutuhumiwa kwa kupindisha ukweli na kujaribu kuficha tabia na mienendo yao wanapozungumza na wapenzi watarajiwa. Naam, katika mazungumzo ya kwanza baina ya wapenzi au wachumba watarajiwa uwongo – ukiwemo ule usiotarajiwa – huwa mwingi.
Katika mazungumzo ya kwanza ni kawaida kwa mwanamume kubadilisha matendo yake na mtindo wake wa kuzungumza kwa maslahi ya kumpata mwanamke, jambo ambalo huifanya hulka yake ya wakati huo kuwa ya bandia. Lakini pia wasichana/wanawake husema “Nakupenda” bila kumaanisha, pengine kwa ajili ya kumfurahisha mwanamume, au kusikia mwanamume atasemaje.
Jambo la muhimu katika mazungumzo ya awali baina ya mwanamume na mwanamke ni kuepuka michezo ya kudanganyana na kukwepana, badala yake, yafanye mazungumzo kuwa rahisi na halisi. Hapo ndipo mwanamume hujitofautisha na wanaume wengine na kupendwa kwa sababu hiyo.
3. USIPUUZE NGUVU YA LUGHA YA MATENDO
Wakati mtu anapokuwa akijaribu kuziwasilisha hisia zake za “Kimapenzi” kwa mlengwa wake, lugha ya matendo yake huzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno yake. Hili limeweza kuthibitishwa kwa nyakati mbalimbali kutokana na tafiti mbalimbali.
Katika muktadha wa kujaribu kufikisha hisia za “kimapenzi” kwa mlengwa, lugha ya matendo ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi. Kwa hakika, asilimia kubwa ya ujumbe unaowasilishwa kwa mlengwa huwasilishwa kwa njia ya matendo ya mwili na si maneno. Ni asilimia ndogo tu ya ujumbe inayowasilishwa kwa maneno – na wakati mwingine maneno huweza kuleta matatizo maana katika kuzungumza kuna kujikwaa kwingi, kwani ulimi hauna mfupa.
Ili uweze kufanikiwa katika kueleza nia yako kwa mwanamke, lazima ujue jinsi ya kutumia lugha ya matendo yako. Na pengine hutatumia nguvu, maana watu husema penzi kikohozi – kwa maana huwezi kuficha kama unalo litaonekana tu machoni pa mlengwa.
Ukitafakari kwa makini utabaini kuwa huhitaji kusema sana ndipo uweze kupendwa, kwani maneno huchangia asilimia kidogo tu. La muhimu ni kuhakikisha kuwa mlengwa wako anakusoma na kukuelewa vizuri kwa kuangalia matendo ya mwili wako.
4. ACHA ASILI ICHUKUE MKONDO WAKE
Katika nadharia mbalimbali za kijamii na kidini ni jambo la kawaida kusikia kuwa binadamu wote ni sawa. Hata hivyo, katika muktadha wa kimapenzi, kila mtu anafahamu kabisa kuwa si kila mwanamume/mwanamke ni sawa na mwenzake.
Methali yenye asili ya kimagharibi husema “Uzuri wa mtu uko katika macho ya yule anayemtazama.” Hii ina maana pia kwamba, kila mtu anavyo vigezo vyake vya uzuri kwa kuzingatia maumbile yake. Pia jamii zinavyo vigezo vya uzuri, lakini hutangulia kwanza vigezo binafsi.
Unapokuwa umekaa na mwanamke ambaye anakuvutia kwa mwonekano wake, sauti yake na kadhalika, si rahisi sana kujizuia kuonesha kuwa anakuvutia. Hii ni kwa sababu si wewe, bali ni nafsi yako inayokusukuma. Na yeye mwenyewe atakusoma kwa kuangalia lugha ya matendo yako na kukwelewa, utakaobaki ni uamuzi wake tu.
Katika jamii kuna vigezo kuhusiana na kiuno, miguu, maziwa, makalio na kadhalika. Wengi wa wanajamii huvizingatia na kuongeza vyao. Huu ni ukweli wa kibiolojia ambao hauwezi kupingika. Mwanamke mwenye vigezo vinavyokubalika zaidi katika jamii yake atawavutia wanaume wengi zaidi. Hapa mwanamume hahitaji kutumia nguvu nyingi – asili ya maumbile itamsaidia humtambulisha mwanamke kuwa amempenda.
5. TUMIA CHANGAMOTO YA WALAKINI
Mara nyingi changamoto kubwa katika suala zima la mtu kubainisha nia yake kwa mwanamke hutokana na ukweli kwamba katika mchakato mzima huwa kuna wasiwasi na walakini. Kwa hakika, jambo hili ni la “pengine” au “labda” kutokana na kutoweza kufahamu kirahisi mwenzako anawaza nini.
Unapoonesha nia yako ya kumpenda mwanamke, ni kama unaamsha hisia zake kwako na ni kama vile unamuuliza: “Ungependa kuwa nami?” Kwa njia hii ni kama utakuwa unafungua mlango wa kupata jibu la “ndiyo” au “hapana” kwani huyo unayemwonesha kuwa unampenda na yeye ana matakwa yake na mapendeleo yake.
Kimsingi hakuna kanuni wala sheria rasmi unazopaswa kuzingatia wakati wote. La muhimu ni wewe mwenyewe kujiachia na kuingia katika maji usiyoyafahamu kina na wala mwisho wake, bali wewe nenda na mkondo wake huku ukitarajia kuwa lolote linaweza kutokea. Hiyo ndiyo sehemu ya raha yake.
6. DHIBITI HISIA, MIHEMKO
Tofauti na mwanamke, mwanamume anayejaribu kuonesha hisia zake hatakiwi kujiweka katika mkao wa mwanamitindo. Wanawake ndio hufahamika zaidi kwa mikao yao “ya kula” wanapokuwa katika mawindo (japo wengi hubisha), lakini si mwanamume. Wanawake ndio hutarajiwa kujieleza zaidi kwa njia ya matendo na mikao, lakini wanaume hutarajiwa kudhibiti hisia na mihemko yao.
Tofauti katika lugha ya matendo baina ya watu wa jinsia mbili hutokana na maumbile ya kujenetiki pamoja na utamaduni wa jamii husika. Yote yakizingatiwa, matakwa ya mwanamke ndiyo hupewa kipaumbele zaidi. Kwa ufupi, matendo ya “kutongoza” ya mwanamke huwa wazi zaidi, lakini mwanamume hulazimika kuficha hisia na mihemko yake.
@IFAHAMU SAYANSI HII
Wajibu wa kufikisha ujumbe kwa mtu wa jinsia tofauti ni wa kila mmoja – mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, wanaume ndio wenye jukumu kubwa zaidi la kuanzisha, kwa kuzingatia utamaduni wa jamii nyingi. Unaweza ukaona ugumu, lakini ipo sayansi itakayokusaidia. Kama una wasiwasi na uwezo wako, ni vizuri kuyazingatia yote yaliyobainishwa hapa.
Share:

KWA WADADA! Dalili 8 za mwanaume mwenye aibu na amekuzimia na Hataki kukwambia

Picha: Mrembo huyu ana hips kubwa na umbo la kuvutia kuliko wote ...
Ukweli usemwe. Kila mwanamume ameumbwa kivyake. Kuna wale ambao mambo yao hupenda kuyaweka wazi na wengine ambao mambo yao hupenda kuyatia kikapuni. Kuna wale ambao hawapendi kujionyesha hadharani na kuna wale ambao mambo yao huyaweka kimbelembele.
Tukija maswala ya kutongoza, kuna mitindo tofauti tofauti ambayo wanaume hutumia ili kufaniikisha lengo lao. Kuna ule msemo unaosema 'mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani, yaani unaweza kufuata njia tofauti tofauti kufika pahali lakini mwishowe utarudi pale pale sehemu moja, so kwa wanaume kila mmoja ana mbinu yake ya kutongoza. Usiwahi kusema kuwa mwanamume aibu hajui kutongoza akiwa na wewe, labda hio aibu yake ni moja wa mtego aliouweka spesheli wa kukunasa wewe.
So utajuaje kama mwanaume mwenye aibu amekuzimia lakini hataki kuonyesha?
1. Anaingiwa na wasiwasi akiwa na wewe
Ukiona mwanaume anaingiwa na kibaridi ama kupapatika akiwa kando yako ujue ni ishara ya kukuambia kuwa amekuzimia. Hii inatokea wakati mko pamoja halafu anaingiwa na wasiwasi mara anafanya hivi mara vile.
2. Anapenda kuulizia marafiki zako kukuhusu
Mwanaume mwenye aibu akikupenda huwa anataka kukufahamu zaidi kukuhusu. Iwapo atashindwa kuongea na wewe moja kwa moja basi ataanza kuwaulizia marafiki zake kukuhusu. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii ya kuulizia marafiki zako, lile la kufanya nikuonyesha ishara za kuwa uko huru kuongea nayeye wakati wowote ule anapojiskia huru.
3. Anakuwa na tabia isiyoeleweka akikuona
Owk wakati mwingine inatokea ya kuwa mwanaume mwenye aibu anashindwa kustahimili kuonyesha hisia zake hivyo kujaribu kuzificha ili usiweze kuzitambua. Lakini badala ya kuzificha, huibua tabia nyingine ambazo hazina mfanano wa kwake. Usishtuke ukiona akifanyika mambo ambayo si ya kawaida manake wewe ndio chanzo kikuu cha kufanyika hivyo. Yaani utakuwa umempagawisha kiasi cha kuwa anaweza kuanza kuchora miduara kwa mchanga akitumia miguu yake.
5. Anapenda kutabasamu na wewe
Wanaume wote kawaida wakipendezwa na mwanamke huwa wanatabasamu. Lakini kwa mwanaume mwenye aibu aliyekupenda huwa tabasamu lake ni tofauti. Mara nyingi atakuwa akitabasamu lakini mara kwa mara anashindwa kukuangalia usoni. Labda anaweza kukuangalia lakini pindi utakapomuangalia yeye atajifanya anaagalia kando. Hii ni baadhi ya tabia ya wanaume wa aibu hufanya wakati anapojaribu kukupendeza.
6. Anakuwa kimya ukiwa naye
Anaweza kuwa anaongea na marafiki zake sehemu flani, lakini pindi utakapotokea ananyamaza kabisa ama kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka. Hata usishangae iwapo atakataa kujibu salam zako kama umempata katika hali kama hii. Mara nyingi ukimkuta akiwa na maongezi na marafiki zake, atajifanya hata hakuwa akizungumza katika kuchangia maongezi.
7. Anabadilisha mwonekano wake
Ukiona kuwa mwanaume mwenye aibu ameanza kubadilisha mionekano yake kwa kuanza kuvalia nguo tofauti, mitindo mipya ya nywele nk akiwa na wewe, jua hii ni ishara ya haraka kuonyesha kuwa amekuzimia. Kufanya hivi kwa kawaida ana makusudio ya kukuridhisha wewe. Labda anadhania ya kuwa kuna mtindo fulani ambao akiuvaa unakupendeza.
8. Anagugumiza akiongea na wewe
Mwanaume huyu hujamsikia akikwamakwama wakati anapoongea lakini ghafla unamskia akigugumiza anapoongea na wewe. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anaishiwa na maneno ya kukuambia na inakuwa vigumu kwake kuyatoa ama kutafuta maneno ya kukuambia.
So ni kitu gani kinachowafanya wanaume aina hii kuwa spesho kwa mwanamke?
Kuna wanawake ambao wanapenda wanaume ambao ni wa aibu kwa kuwa hawana mambo mengi. Lakini usishangae kumwona mwanaume aina hii akikuapproach akutoe mkale bata pamoja. Pia aina hii ya wanaume itafikia wakati fulani wanaweza kukushangaza kwa kufunguka na kugundua kuwa ilikuwa tu ni baadhi ya mbinu waliyotumia kukuteka kimapenzi.
Share:

Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke Kwa Njia Ya Kirafiki

Beautiful gospel artiste confesses she struggles with 's@x' addiction
Wakati unapotongoza mwanamke huwa kuna vitu viwili; aidha unatongoza njia sawa ama unatongoza kwa kubahatisha.
Njia yeyote katika hizi mbili utakazozichukua, mwanamke atafahamu ya kuwa unajaribu kumpendeza na anajua unataka kutoka naye deti.
So matumaini yako hapo ni kuona ya kuwa mwanamke kama huyu anavutiwa na wewe bila kukukatiza tamaa.
Ok, unless huyu mwanamke anatafuta mchumba wa kudeti ama anatafuta mwanaume wa kujikeep naye buzy, kuna nafasi kuu akigundua ya kuwa unabahatisha kumtongoza, papo hapo atakuzima na kukuonyesha dalili za kuwa hakupendezwa na njia yako ya kujaribu kumuapproach.Akikukataa najua unaweza kuingiwa na misongo ya mawazo kutaka kujua kwa nini amekukataa. Unaweza kusumbuliwa na jambo hili kwa muda mrefu.
Lakini kama kawaida, kutongoza mwanamke huwa ni bahati nasibu, anaweza kukukubali ama kukukataa.
Well, leo nimeamua kuja na mbinu tofauti ya kutongoza mwanamke. Hii mbinu itamfanya mwanamke kuingiwa na maswali ya kujiuliza iwapo unamtongoza au la. Mbinu hii utamvutia mwanamke bila hata kumwambia neno "NAKUPENDA".
Zama nami
Jinsi ya kumtongoza mwanamke kiurafiki
1. Kuwa mwanaume bora
Katika dunia tunayoiishi sahizi kila mwanaume anatamani kuwa na mwanamke bora zaidi. Hivyo kutaka kuwa na mwanamke unayempenda lazima uwe bora kuliko wengine. Hii ni kuanzia tabia zako, vile unavyohusiana na wengine, miondoko yako, unadhifu wako nk. Kuwa mwanaume bora hakuna njia ya mkato. Lazima ufuate mkondo ambao wengi hawaufahamu.
2. Msifu vile inavyotakikana
Leo amekuwa tofauti kimwonekano?, ama leo amebadilisha hairstyle yake? Kama umependezwa na mwanamke mara nyingi utakuwa unanotice mabadiliko yeyote ambayo ameyafanya hivyo chukua nafasi yako kumsifia vile inavyotakikana.
Well, sasa kama unataka kumvutia ili umuingize katika mipaka ya kudeti unafaa utumie maneno ambayo hatoyasahau. Usitumie maneno ya kawaida. Jaribu kutumia maneno ambayo hayatasahaulika kwake na ambayo ni ya kibinafsi bila kuvuka mipaka. Mfano wa maneno kutumia:
Hilo shati ulilovaa ni zuri - linakufanya unapendeza zaidi ya tausi
Marashi mazuri - leo unanukia utamu ambao sijawahi kuunusa popote
Unaweza kumsifia mwanamke chochote kile ilimradi pindi utakapotamka tumia maneno ya kibinafsi. Hii itamfanya wakati mwingine atakapopaka marashi hayo atakumbuka maneno uliyoyasema. Kufanya hivi kunamvuta polepole na kukufanya wewe kuingia katika moyo wake.
Kutumia maneno kama "ngozi yako ni laini, hivi wakati wote unakuwa hivi?" ama "nimependa shati lako na vile jinsi limekubana katika mwili wako" hakufai. Kusifu kwa aina hii usithubutu kutumia kwa sasa kwani unaweza kuharibu mpango mzima.
3. Tafuta muda wa kuwa nyinyi peke yenu
Kumsuka mwanamke huwa ni bora zaidi wakati ambapo mko nyinyi wawili pekeenu. Kumsuka mwanamke mbele ya marafiki zako kutamfanya kukuona wewe hauko serious na mambo unayotamka hivyo ni bora wakati ambapo unachukua muda na kuwa na yeye pekeenu mnaongea.
Unaweza kumsuka kwa kutumia mizaha wakati ambapo mko na marafiki zenu. Lakini wakati ambapo mko nyinyi wawili, tumia maneno ambayo hatayasahau kiurahisi. Mfano unaweza kumwambia "wewe ndie unafanya siku yangu kuwa ya shangwe", "kukaa na wewe hapa najiskia niko huru" nk kutamfanya yeye kujiona spesho kwako.
Ujanja hapa ni kutumia maneno ambayo yatamfanya yeye kujiona spesho kuliko yeyote na amini usiamini mwanamke kama huyu atakuwa akifikiria mazungumzo yenu kwa muda mrefu.
4. Wanawake wanapenda ucheshi
Hivi wewe ni mcheshi? Kama jibu lako ni la basi usiendelee kusoma zaidi ya hapa mpaka uifahamu sanaa ya ucheshi.
Nadhani unafahamu ya kuwa njia ya kumvutia mwanamke lazima utumie lugha ya ucheshi mara kwa mara. Well, uzuri ni kuwa si lazima uwe na ustadi wa kuchekesha. Unaweza kuelezea matukio yako ya awali ambayo uliona yalikuchekesha. Kama mwanamke anaonyesha dalili za kukupenda, basi kila neno utakalolitoa kiutani atacheka.5. Msumbue mara kwa mara
Wakati mwingine kumsuka mwanamke kunaweza kuonekana kuwa ni kazi ngumu, lakini kitu muhimu ni yale mambo madogo madogo ambayo mnafanya. Kumsuka mwanamke si kutumia maneno matamu ya kimapenzi pekee bali pia zile tabia ambazo mnafanya wakati mnapokuwa mnaongea. Hii ni kuanzia kucheka hadi migusano yenu ya mara kwa mara.
Kama nyote wawili mnakuwa na furaha wakati mnapoongea, hio tayari ni njia moja rahisi ya kuashiria unamsuka. So kuivuka mipaka ya urafiki, unafaa kuivuta miguu yake mara kwa mara upande wako wakati ambapo ameongea kitu cha kuchekesha ama mnapocheka. [Soma: Jinsi ya kumpandisha nyege mwanamke bila kumfanya kitu]
6. Cheza na mazungumzo machafu
Hatua tano za awali ambazo tumezitaja ni za kujenga mazingira ambayo yanawaweka katika hali ya kuleta nafasi ya kusukana kiurafiki.
Wakati ambapo utachagua kuvuka hii hatua, nyote wawili mtakuwa mumeingia hatua ya kuanza kutongozana.
Wakati ambapo umepata nafasi ya faragha ama unapompigia simu, jifunze kuchanganya maneno yako. Kufikia sasa najua nyote wawili kuna tenshen flani ambayo itakuwa imejijenga kati yenu hivyo usiingiwe na wasiwasi kama utajaribu kuingiza maneno ambayo yamevuka mipaka. Mara moja au nyingine unaweza kuingiza maneno ya kimapenzi katika mazungumzo yenu. Hata kama atakwambia uachane na hayo maneno utakuwa umechukua hatua kubwa kuonyesha hisia zako kwake.
7. Leta hisia za mguso
Wakati unapomsuka mwanamke ni vizuri zaidi kama utatumia sanaa ya miguso. Mara kwa mara tafuta kisababu cha kumgusa. Aidha unaweza kumgusa viganja vyake, mikono, vipuli vyake nk. Na kila wakati ambapo utakuwa ukimgusa hakikisha unachukua muda wako kumgusa ili ahisi mkono wako kwa mwili wake. Kufanya hivi atakuwa akipenda kama utatumia mbinu ya kijanja.
8. Muombe mtoke out mara kwa mara
Mara moja wakati wa maongezi yenu unaweza kumuomba umtoe mwende mkahawani ama kumpeleka katika sinema siku ya pili. Wakati mzuri wa kumwambia haya ni wakati ambapo mmemaliza maongezi yenu ama wakati mnapokuwa mnatext. Kumuuliza hivi si lazima uonekane uko serious na vile unavyosema. Kumaliza maongezi yenu kwa ghafla kutamwacha mwanamke kama huyu kujiuliza maswali iwapo ulikuwa uko serious wakati wa kumwambia wataka mtoke out ama ilikuwa tu mizaha.
Siku ya pili mkumbushe tena kuhusu deti yenu lakini usionyeshe kama uko serious. Kama atacheka pia wewe cheka halafu ujeuze mada. Labda atakuwa hajui kama uko serious ama ni mzaha ama bado hajapenda wazo la kwako kutoka deti na wewe.
Kama atakubaliana na mwitikio wako, kila la heri kwako. Iwapo atakataa basi anza tena mikakati yako ya kumridhisha mpaka aingiliane.
NB: Mara nyingi kama utafuata hatua za awali vizuri, mwanamke kama huyu hawezi kukataa mwitikio wako.
9. Zile simu za usiku wa kiza
Usiku huwa na mbinu ya kufurahisha kuamsha hisia zetu za mapenzi.
Marafiki wowote wawili ambao wanaongea kwa muda mrefu nyakati hizi za kiza mara nyingi hufikia hatua hii. Kama wataka kujua jinsi ya kutongoza mwanamke ili akupende chukua nafasi ya kumpigia simu ama kumtext nyakati kama hizi. Hakikisha ya kuwa unamrushia maneno ya kumtongoza.
Wakati huu wa usiku ambao umetulia ukiwa unaendelea na maongezi yenu ni rahisi sana kwenu kuivuka mipaka ya kuwa marafiki na kuanza kuonyeshana hisia zenu za mapenzi.
10. Mwonyeshe kuwa wewe unaweza kuwa mwenza mzuri wa kudeti
Ok kufikia sasa utakuwa umeshamwonyesha hisia zako zote, umemvutia na kujenga kemia za kimapenzi kati yenu, lakini utakuwa bado hujafunga mchezo. Atakuwa labda amependezwa na maongezi yenu na pia kukupenda kisiri, lakini kumfanya mwanamke akuone wewe kama una nafasi nzuri ya kuwa mwenza wake lazima uonyeshe dalili.
Wakati wa mazungumzo yenu, unaweza kutoa fununu za kuwa unatafuta girlfiriend ama unatafuta mwanamke wa kutoka naye out. Kama yuko single ama katika mahusiano mabaya, kitu kitakachokuja akilini mwake ni wewe na yeye katika hali kama hio, mwanzo itakuwa bora kama utachukua nafasi ya kuongea haya yote nyakati hizi za kiza.
Pindi utakapojua kutumia mbinu hii ya kutongoza mwanamke kiurafiki, kazi yako itakuwa imerahisishwa ya kutongoza kwani utakuwa ukitumia mbinu ambayo si ya kubahatisha.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU