-->

Wanaume Hutongoza Wanawake Wanaowaona; Hii ndiyo sababu ya kwanza ya mwanaume kumtongoza mwanamke.

Wanaume Hutongoza Wanawake Wanaowaona; Hii ndiyo sababu ya kwanza ya mwanaume kumtongoza mwanamke, kwamba ili wewe mwanamke uitwe na mwanaume akuombe namba yako ya simu na kukutongoza, nilazima huyo mwanaume akuone kwanza, kwamba hata kama umzuri kama Malaika kama unajifungia ndani basi hutapata mtu wa kukutongoza hivyo hutapata mume!
Labda nifafanue kidogo, hembu angalia ratiba yako wewe mpweke, unaamka asubuhi, unajiandaa unaenda kazini, huko unakua bize na kazi na unaonana na wafanyakazi wenzako ambao washakuzoea waaala huataki na wao hawakutaki! Ukitoka ni kwenye daladala nyumbani, huko unakaa weekend wewe ni kujifungia ndani.
Sasa watu unaokutana nao ni wafanyakazi wenzako ambao tayari mshazoeana nao na hawakutaki, kwenye dadala kuna watu na stress zao hata hawakuoni, kama una gari ndiyo hata hukutani na mtu! Majirani zako ambao nao wote wameoa au tabia zao ushawachukia! Sasa Dada yangu ukimuomba Mungu akupe mume unataka muoneshe hapo chumbani!
Au unataka utongozwe na Kabati ambalo unashinda nalo kila siku? Ili mwanaume kutongoze nilazima akuone, ukitaka mwanaume mwenye hela nenda sehemu wanapokaa wenye hela, ukitaka mfanyabiashara hivyohivyo, acha kujifungia ndani ukidhani ni tabia nzuri, ukidhani ndiyo wanaume watakutongoza. Kwakua umetulia ukitoka kazini ni nyumbani, umetulia kweli lakini hawakuoni!
Umzuri lakini huwezi kujitongoza mwenyewe, hembu toka na marafiki, hudhuria matukio, toka mwenyewe, nenda sehemu za starehe. Sisemi uwe mtu wa bata hapana lakini nasema utoketoke hata nnje wanaume wakuone wakutongoze, hawawezi kukuonea huko ndani kwako. Tafuta sehemu za kistaraabu nenda utakutana na wastaarabu wenzako watakutongoza na kukuoa!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU