-->

My sister; Sio kwamba wanaume wote ni walaghai,sio kwamba wanaume wote si wenye kujari na kuthamini,

Posh Queen: Mpenzi wangu anapata tabu sana | JamiiForums

My sister;

Sio kwamba wanaume wote ni walaghai,sio kwamba wanaume wote si wenye kujari na kuthamini,sio kwamba wanaume wote wapo kwa ajiri ya ngono na wewe, hapana bali wapo wanaume wenye nia ya dhati na upendo wa kweli kabisa kwako,lakini kutokana na jinsi unavyojiweka wana ogopa hata kukutongoza tu.

Mara nyingi sana mwanaume anapohitaji ndoa basi huhitaji mwanamke ambae ataweza kutengeneza utulivu ndani ya Nyumba,hakuna mwanaume ambae anahitaji mwanamke pasua kichwa ili afunge nae ndoa, sasa my sister kama utajiweka kuwa mke mwema basi utapata mume mwema pia na kama utajiweka kuwa ni mwanamke wa dunia basi tegemea kupata mume wa dunia pia.

Mnaposhindwa kujitunza kujilinda na kuwa na subira mnatengemea nini? Mnategemea kupata waume bora kwenu ikiwa nyie mmeshindwa kuwa wanawake bora, badilikeni hizi tabia mlizonazo sasa za kushindana na dunia,hamuwezi kuolewa au kupata waume bora katika maisha yenu, cha zaidi mtapata wanaume wenye tabia kama zenu.

Jifunze kuwa,mwanamke ukijiheshimu kujithamini na kujipenda utakuwa mke wa daraja la juu sana kwa huyo mwanaume ambae atabahatika kuwa mume wa maisha yako,badilikeni simameni katika tabia za kumpendeza mume.

Share

Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU