-->

MBINU 10 ZA KUFUFUA PENZI LILILOKUFA


Mada ya leo ni maalum kwa watu ambao tayari mpo kwenye uhusiano wa kimapenzi, iwe ni wapenzi wa muda mrefu, wachumba au wanandoa
DALILI ZA PENZI LILILOKUFA
Umewahi kuhisi kwamba penzi lako limefikia mwisho japo bado upo na mpenzi wako, mchumba au mumeo/mkeo? Yaani upoupo tu, zile hisia tamu za mapenzi
ulizokuwa nazo wakati mnayaanza mapenzi yenu hazipo tena, hufurahii kuwa naye, hamzungumzi mkaelewana badala yake kila siku ni ugomvi na migogoro isiyoisha!
Kila unachokisema au atakachokisema hata kama ni kizuri vipi kinakuwa sawa na petroli kwenye moto, kinazidi kuchochea uhasama na chuki kati yenu.
Kila mnapoanza kuzungumza, hata kama ni jambo zuri lazima muishie kutukanana, kufokeana au kupigana.
Unaishi naye nyumba moja lakini kila mmoja analala kwenye chumba chake, hata mkilala pamoja kila mmoja anageukia upande wake, hujisikii chochote juu yake, hata akiugusa mwili wako unaona kero na hutaki hata kumtazama usoni.
Hujisikii hamu tena ya kuwa naye faragha, kila unachokifikiria kuhusu yeye kinakupandisha hasira na kukuudhi!
Unatamani uhusiano wenu ufikie mwisho hata sasa hivi ingawa hujui uanzie wapi,unatamani mwenza wako afe kwa ajali au apate mabalaa makubwa yatakayowatenganisha.
Ukiona hayo yote niliyoyataja na mengine mengi yanakutokea, huo ni uthibitisho kwamba unaishi kwenye mapenz yaliyokufa, Wazungu wanasema Dead Love. Kwa wale ambao wameishi kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu watakuwa wananielewa vizur zaidi, kama upo kwenye penzi jipya, huwez kuelewa vizur
KUACHANA NDIYO SULUHU?
Wengi wanapofikia hatua hii ya kuishi kwenye mapenz yaliyokufa, huwa wanakosea sana kuamin kwamba njia pekee ni kuachana. Hata kama ni wanandoa na walishafanya mambo mengi pamoja ikiwa ni pamoja na kuzaa, wataishia kupeana talaka! Inasikitisha sana.
Hata hivyo, hiyo siyo dawa kwan ni kuyakimbia matatizo!
Utaachana na wangapi? Wataalamu wa mahusiano na mapenz wanasema kila penz lililokomaa, lazima lipitie kwanza kwenye hatua ya kufa, ukwel ambao ni wachache huweza kuukubal
Wahenga wanasema dhahabu ili ing’ae lazima ipitie kwanza kwenye moto
NINI CHA KUFANYA?
1. Hatua ya kwanza, jiwekee nadhir kutoka ndani ya moyo wako kwamba upo tayar kulifufua penzi lako lililokufa
Yawezekana wewe umeamua hivyo lakin mwenzako hayupo tayari, hilo lisikukatishe tamaa
Jiambie moyon kwamba utafanya kila kinachowezekana kurudisha furaha, amani, hisia za mapenzi, msisimko na upendo kama ilivyokuwa wakati mnaanzisha uhusiano wenu
ITAENDELEA..
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU