-->

Katika malengo na mawazo uliyojipangia kichwani mwako, jitahidi kila siku unapiga hatua moja kuyafikia.

Kila ukiamka jijengee mazoea ya kujiuliza nitafanya kitu gani leo ili niweze kufika napotaka.
Mi naamini katika kila hatua moja utayopiga itakupa moyo na kujifunza zaidi juu ya kile unachotaka kukitimiza. Usibaki na mawazo na ndoto zako kichwani tu, maana kila siku utabaki pale pale na mwisho wa siku utakufa moyo kabisa wa kufanya kile unachokipenda.
Najua wakati unaanza hakuna atakayekuelewa, watakuona chizi, utapoteza hela, utapoteza marafiki, utakatishwa tamaa na hata wewe mwenyewe unaweza kupoteza kujiamini kwa kile unachofanya.
Ingawa utayapitia yote hayo, jipe moyo na jiamini kuwa unaweza kuyafikia malengo yako. Wale wasiokuelewa leo ipo siku watakuja kuomba ushauri kwako kukuuliza umewezaje, ipo siku wewe utakuwa mfano kwao na naendelea kukumbusha tu ni marufuku kukata tamaa na amini katika kila hatua ndogo unayoipiga leo.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU