-->

ILI NDOA IWE NA MAFANIKIO, MWANAMUME INABIDI UJITAMBUE ZAIDI


Sababu ya kwanza ya watu kuingia katika mapenzi ni furaha.
Kwa maana hiyo ni jukumu la kila mtu aliye katika uhusiano ni kumfanya mwingine awe na furaha na amani. Mvuto na mali za mtu hazina maana sana kama miongoni mwao hakuna furaha.
Mali na mvuto wa mtu huzidi kuchochea raha ya mahusiano kama kukiwa na furaha.
Nani anaweza kusimama na kusifu mali ama mvuto wa mwandani wake ikiwa kila siku anamfanya kulia na kujutia uamuzi wake?
Maisha ya mahusiano yanadumishwa na amani na furaha.
Kwa sababu hii, ndiyo maana mara zote katika darasa zangu nasisitiza watu waingie katika mahusiano wakiwa wanapendana kwa dhati na si kubabaikiana kutokana na umaarufu ama umiliki wa mali.
Mahusiano yanayojengwa kwa misingi ya mapenzi ya dhati, baadaye huleta heshima na kusikilizana.
Ni katika kusikilizana huko ndipo mtu anaweza kuamua kuacha jambo fulani akihisi linamkwaza mwenzake na kufanya lile ambalo litajenga tabasamu na matumaini kwa mwenzake.
Pamoja na hilo ila pia mahusiano makini ni yale kila mmoja anayojitambua yeye ni nani na majukumu yake kwa mwenzake ni nini. Mfano, mwanamume katika uhusiano ni kiongozi.
Kwa sababu hii, anatakiwa ajue namna gani anaweza kuishi na mwenzake katika namna ya kumwongoza vema bila kumfanya ajihisi yuko utumwani ama jeshini.
Kauli na matendo yake si tu yafanye aonekane ni kiongozi ila pia yawe ni kielelezo sahihi cha uongozi wake na chanzo halisi cha furaha kwa mwenzake.
Pia mwanamume anapaswa kujua, popote alipo kiongozi, basi huwa kuna mwongozwa.
Basi kwa hivyo, inabidi ajikite katika nafsi ya uvumilivu ama uonyaji wenye staha.
Mwanaume anatakiwa ajue mwanamke ni kiumbe anayetakiwa mara nyingi kuoneshwa njia. Hivyo badala ya kugombana kidogo, yeye awe wa kwanza kukimbilia kusema tuachane, awe mwalimu mwema na kiongozi bora kwa mwenzake.
Kuitwa kichwa cha familia mwanaume maana si tu kupikiwa chakula na kuacha fedha ya matumizi. Ni zaidi ya hapo.
Mwanamume anayejitambua anatakiwa kuishi na mwanamke kwa uvumilivu huku akimsoma na kujua namna gani anaweza kumfanya awe anavyotaka yeye.
Mwanamume hupaswi kulalamika hovyo hata kipindi unachokosewa.
Badala yake kaa jiulize ni kipi kimefanya mhusika kufanya aliyoyafanya.
Ni kweli kwa sababu hakupendi ama ni kutokana na uelewa wake kuwa mdogo katika jambo husika?
Mjanja hapaswi kukimbilia katika kupiga na kutoa vitisho.
Kwani katika ndoa vitisho na vipigo havijawahi kuwa suluhisho la matatizo hata kidogo.
ITAENDELEAA..✍️✍️
UTAMU KITANDANI APP
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU