🍓Naomba ujifunze hili iwapo Mtu anapokufanya wewe kama wa akiba, msaidie kupunguza akiba yake kwa kumuondoa kwenye maisha yako.
🍓Muda mwingine wewe nawe lazima uwe na ujasiri wa kuonyesha kuwa haujali, bila ya kuangalia ni kwa kiasi gani unajali!
🍓Kwa sababu inatokea muda mwingine mtu anakuona huna lolote wakati wewe unamuona ni kila kitu kwako!
🍓Kufanya hivyo sio kwamba unajisikia na unaringa, Hapana. bali ni kwamba unajiheshimu na zaidi unarudisha hadhi, thamani na utu wako!
🍓Usitarajie kuona mabadiliko yoyote chanya katika maisha kama bado unazungukwa na watu wenye mawazo hasi juu yako na wasioongeza thamani katika maisha yako!!
🍓Usiwape nafasi watu wa muda mfupi katika maisha yako. Fahamu thamani uliyonayo, na usikubali kupokea kidogo au kutopokea kabisa wakati unastahili kupokea makubwa zaidi ya hayo unayopewa!