-->

USIMLINGANISHE MKEO NA MCHEPUKO WAKO.


Wanaume Wenzangu Naomba Mnisikilize kwa Umakini hapa.
Hivi mke wako Anawezaje Kuwa sawa Na Mchepuko wako ? Au wakati mwingine Unasema Mkeo Sio mrembo kama mchepuko wako kwanini lakini?
Hebu Angalia, umempa ujauzito mara 3 au 4 wengine mpaka mara 6 na zaidi,Ameingia Leba kukuzalia watoto mara zote hizo na ameendelea kukupenda tu.
Mkeo anapitia taabu nyingi wakati anapokuwa mjamzito, wakati mwingi analala upande upande kwa sababu ya kiumbe chako kilichokuwa tumboni mwake.
Akisha jifungua anapambana kunyonyesha na kukulelea watoto wako mpaka wanafikia umri wa kuondoka nyumbani, anakupikia , anakufulia na kukufanyia shuhuli zote za nyumban je mchepuko wako ungeweza yote hayo ??
Mara nyingi mke wako amelazwa hospitali kwa ajili ya watoto wako lakini bado yupo ngangari anapambana.
Wakati mwingine Amechanwa tumbo lake kwa kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida lakini bado yupo sawa anatabasamu siku zote.
Ulimchukua mtoto wa watu ngozi nyororo , na bado mrembo lakini kutokana na kukubebea wanao na kukulelea kwa kuwanyonyesha maziwa yake yamelala, amepata michirizi isiyoisha katika tumbo lake yote sababu yako na wanao.
Wakati alipokuwa mjamzito alishindwa kula, mara nyingi alikuwa anatapika, umemchukua mtoto wa watu unamfungia ndani haruhusiwi hata kufanya kazi maana ulimwachisha ili awe wa kukulea wewe na watoto wako Lakini bado unashindwa kumuheshimu.
Hebu Mchukue Mchepuko wako Umuweke katika Hii Safari ambayo mke wako amepitia na bado anaipitia uone kama ataweza kuifanya kwa ubora kama mke wako.
Niwaombe tu Kaka Na Ndugu Zangu Jifunzeni Kuwaheshimu na Kuwapenda Wake zenu. Jaribuni kukumbuka kwamba ni kwa sababu yetu wanaume wanawake wanapitia Dhahama zote hizo.
Tuache kuwaheshimu michepuko inayopanua miguu kwa ajili ya pesa na kuwadharau wake zetu wanaokubali kupoteza urembo,uzuri,kutulea na watoto wetu na hata kututii na kutuvumilia katika shida na raha....!
Pata Hofu ya Mungu Muheshimu mkeo anayekupenda kwa dhati ndiyo maana alikubali kuolewa na wewe ingawa ulikuwa huna kitu! Na Mungu atakubariki!!
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU