Moja ya kanuni kubwa ya kutongoza nikuwa, kama mwanamke anaendelea kukujibu, hata kama ni kwa kukutukana au kukuambia kuwa sitaki basi jua kuwa anakutaka au ana mpango wa kukubali. Mwanamke ambaye hana mpango na wewe basi hukupuuzia, kwamba ukimtumia meseji kwanza hajibu na pili anakublock kwa usumbufu na kama wewe ni king’ang’anizi basi ukipiga simu anaweza kupokea na kukuwekea muziki akaacha uongee mpaka uchoke kama chizi.
Lakini kama mwanamke anapokea simu yako, anakujibu kwa kukutukana, kama Baharia unaamini kuwa ipo siku atakubali. Hii ndiyo mamaa mwanaume yeyote mzoefu akikuta meseji za mwanaume mwingine katika simu ya mke/mpenzi wake haangalii alichoandika Baharia mwenzake bali huangalia majibu. Akiona mwanamke wake kajibu anajua kwa hapa kuna kitu, anahisi kaona manyoya huyu kuku atakua kashanyonyolewa.
Nilichotaka kusema hapa dada zangu nikuwa, kama mwanaume humtaki kuna haja gani ya kujibu mseji yake. Yaani ashakutongoza mara moja ukamuambia sikutaki, kwanini mara ya pili. Unavyorudiarudia ni kama unamkaribisha kuendelea kukusumbua. Yeye anaona ni mchezo tu, kama humtaki, mjibu mara moja, futa meseji zake, kisha block akizidi kusumbua acha kuzisoma basi muache apige pokea weka chini kaoshe vyombo. Lakini kama unamjibu hata kama ni matusi basi unamtaka, narudia kama unamjibu unamtaka.
Naomba nirudie kama unamjibu hata kama ni matusi unamtaka ndiyo maana unampa muda wako. Unakuta mwingine eti anakuambia “Nilikua namuelezea kuwa simtaki!” Pumbavu, sikutaki ni sikutaki inahitaji maelezo gani mengine hapo? Najua kuna ambao mtasoma hapa na hamtaamini mpaka muachwe. Ila Baharia ukiona mpenzi/mke wako anachata na mwanaume ambaye anamtukana kila siku na anasema hamtaki, jua ni suala la muda tu utakuta manyoya!