-->

NDOA NI SAFARI HIVYO JALI SAFARI YAKO

Kwenye mapenzi ukiona mtu anamsifia na kumuongelea vizuri sana mume au mke wake, haimaanishi kwamba huyo anayesifiwa ni mkamilifu au yuko perfect, na kama ulidhania hivyo basi akili yako ina shida kidogo.
Iko hivi, kwenye mapenzi hatutafuti au kuishi na mtu mkamilifu bali mtu ambaye mazuri yake yanazidi maradufu madhaifu yake na yale madhaifu hayana nafasi kuathiri mtazamo wa huyu anayesifia.
Kwenye mapenzi tunatafuta anayebebeka na kuvumilika maana hayo ya kuvumilika kwake hayazidi yale yasiyovumilika, nasema hivi maana wapo ambao hawabebeki, hawachukuliki na hawavumiliki kwa jua wala kwa mvua.
Yamkini hawa ndio wale ambao huzitamani ndoa za wenzao, huwatamani wake na waume wa wenzao na hupandwa na povu sana wanapoona mtu anamsifia mwenza wake.
Ndoa ni safari, hivyo jali safari yako.
Share
Like Page
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU