-->

Maana halisi ya neno mnafiki ni kama kama ifuatavyo;


✓✓Mnafiki ni mtu anayesema kinyume na anavyotenda.
✓✓Mnafiki ni mtu anayetoa ahadi kisha asitimize.
✓✓Mnafiki ni mtu mwenye tabia ya kutokusema ukweli.
✓✓Mnafiki ni yule mtu anayefanya jambo ambalo anajua kabisa kwamba sio la kweli.
✓✓Mnafiki ni mtu yule anayetumia hila kwa lengo la kujinufaisha yeye.
Hizo ndizo maana halisi za mtu mnafiki haijalishi anamuonekano gani.
Haijalishi ana madaraka gani.
Haijalishi anapendwa na watu kiasi gani.
Haijalishi ana ishi wapi.
Luka 6:42-44 ''Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? MNAFIKI wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.''
-Biblia haimhitaji mnafiki.
-Mkristo hatakiwe kuwa mnafiki.
-Mkristo hatakiwi kutamka unafiki.
-Kama wewe ni mnafiki hakikisha kwanza unatubu na kujifungua kutoka katika vifungo vya unafiki ulionao ili uwe mwema ndipo utakapoweza kuwa baraka kwa wengine.
Kuna mifano mingi ya unafiki iliyofanywa na baadhi ya watu zamani.
Kaini alifanya unafiki kwa Habili ili amuue na akamuua na kuleta laana kubwa maishani mwake.
Unafiki mwingi unaangamiza maisha ya wengine leo.
Delila alifanya unafiki wa upendo kwa Samson hadi ikapelekea Samsoni Kutobolewa macho.
Unafiki ni kitu kibaya sana.
Unafiki hautakiwi kuwapo katika watu wa MUNGU waliookolewa kwa Neema ya Bwana YESU.
Unafiki ni lazima uwe mbali na nyumba ya MUNGU.
Zaburi 12:2-3 ''Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;''
Unafiki ni machukizo kwa MUNGU.
Mtu aliyeamua kumpendeza MUNGU anatakiwa asiwe na unafiki wowote ndani yake.
unafiki umeleta madhara mengi katika watu wa MUNGU.
Mchumba "mnafiki" amesababisha maumivu makubwa kwa mwenzake waliokuwa pamoja kama wachumba kisha kuachana.
Watumishi "wanafiki" wameitukanisha injili kwa sababu ya uongo wao na hila zao.
Unafiki ni pando la shetani linalotesa wengi sana, ujumbe wa leo unakataza mkristo kuwa mnafiki maana unafiki ni machukizo kwa MUNGU.
Mithali 12:20 '' Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.''
Ndani ya unafiki siku zote kuna uongo.
Ndani ya unafiki siku zote kuna hila na ndani ya unafiki siku zote kuna pando la shetani.
Ndugu zangu, hakuna haja ya kuwa mnafiki ili hali unatakiwa kuwa mkweli daima.
usiseme unafiki na wala usijiunge na watu wasemao unafiki.
Kataa kuwa mnafiki kwa kuamua kuwa mkweli tu katika kila jambo ulitendalo.
Yeremia 3:9-10 ''Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti. Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki, asema BWANA. ''
-Hili ni Neno la unabii ambalo linaonyesha waisraeli katika muunganiko wao walivyokuwa wanamrudia MUNGU kwa unafiki.
Hata leo kuna watu hurudi kanisani kwa unafiki.
Kuna watu huenda kanisani kwa unafiki.
Kuna watu hufanya mambo fulani kwa unafiki ili tu wasifiwe au wapate kibali fulani.
Ndugu, Hakuna haja ya kuwa mnafiki wakati kuwa mkweli inawezekana.
Kuna watu leo huchumbia kwa unafiki kisha kuwalaghai wachumba zao kwa kuzini nao kisha kuwaacha.
Kuna Wanandoa leo hujifanya wanawapenda sana wenzi wao wa ndoa kumbe ni wanafiki wakubwa maana husaliti ndoa zao.
Mkristo Hatakiwi kuwa mnafiki katika jambo lolote.
Kataa unafiki katika maisha yako.
Bwana YESU anawaonya mafalisayo ambao ni sehemu ya wanadamu kama ulivyo wewe akisema;
''Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.-Mathayo 23:27-28 ''
-Ninyi mnaonekana kwa nje kama watu wenye haki kumbe ndani ni wanafiki.
Hata leo kuna watu kwa nje huonekana ni wenye haki lakini ukweli halisi watu hawa ni wanafiki.
Kuna watu huonekana kwa nje ni watakatifu lakini ukweli ni kwamba ni wadhambi wakubwa, huo ni unafiki.
Kuna watu hupewa hata tuzo za utakatifu na wanadamu wenzao lakini kumbe hata hawafanani na utakatifu hata kidogo.
Unafiki ni bidhaa ya shetani inayotakiwa kuondolewa katika kanisa la MUNGU.
Mnafiki ni mtu mwenye tabia ya unafiki.
Na maana halisi ya unafiki ni;
Unafiki ni hali ya mtu kujifanya ni rafiki lakini kumbe ni adui.
Unafiki ni hali ya kutokuwa mkweli.
Mkristo hatakiwi kuwa mnafiki.
Biblia inasema '' Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa MUNGU; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika ROHO MTAKATIFU, katika upendo usio unafiki;-2Kor 6:3-6''
-Inatakiwa kuwepo upendo usio na unafiki.
Inatakiwa siku zote yatendeke matendo mema yasio na unafiki.
Inatakiwa isimame kweli siku zote na sio unafiki.
2 Kor 4:1-2 '' Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei; lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU.''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Peter M M

Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU