-->

JIFUNZE KUJUA WAKATI WA KUACHANA NA WENGINE UNAPOFIKIA SIO KILA MTU UTADUMU NAYE KWA MUDA WOTE..

...Pix for my column - olayemiogunojo.com
Kuna watu wataanza na wewe wanakusaidia kufika mahali fulani Kisha wataondoka kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wengine' wape fursa ya kuwasaidia wengine pia usiwe mbinafsi kuwang'ang'ania.
Kuna watu walikuja ili uwasaidie wakishaimarika wanaendelea na Safari na wewe endelea na Safari yako' usinung'unike kuwa hawako na wewe tena' furahia mafanikio yao mungu alikutumia kuwasogeza hatua usitake kuwamiliki.
Kuna watu walikuja kukufundisha kitu fulani ukishapata somo wanaondoka' inaweza kuwa kupitia maumivu ama furaha ila somo utalipata wanakusaidia kukuongezea umakini katika maisha yako.
Kuna wengine walikuja ili wakuunganishe na watu wengine' wakishamaliza wanaondoka wanaweza wasikupe kitu ila wakakuunganisha na mtu ama watu/ fursa itakayokufanikisha.
Kuna wengine walikuja kukuharibia mwelekeo wakishakutoa kwenye mstari' wanaondoka furaha yao na ushindi wao ni kuona umepoteza mwelekeo.
Kuna watu wamekuja kwasababu kuna msimu mpya wa maisha yako' msimu huo ukishapita na wao wanakuwa wamemaliza kazi, ni marafiki wa msimu.
Kuna watu walikuja kwasababu kuna kitu walitarajia kukipata kutoka kwako' wakishakipata tu wanaondoka hawana cha kukupa hawa, usijaribu kutarajia kutoka kwao.
#kunamudahatasimuyakoyawezakukupafuraha
🖕🖕🖕
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU