-->

IJUE TOFAUTI YA NDOA NA HARUSI


Ndoa ni AGANO LA MUNGU KWA WAWILI WANAOAMUA KUUACHA UZINZIπŸ“–
kwani hata Mtume paulo alipata kusema;
"MNGELIKUWA KAMA MIMI BASI MSINGESUMBUKA NA HILO ILA KWAKUWA HAMKO KAMA MIMI BASI KILA MMOJA NA AWE NA WA KWAKE"
Ukirudi kwenye maana ya HARUSI ni tendo la kusheherekea wawili walioamua kudhihirisha kwamba WAMEAMUA KUWA PAMOJA MBELE YA USHUHUDA WA UMATI AMA JAMII.
Kwa ufafanuzi huo unabaini kwamba NDOA ni KIFUNGO na HARUSI ni tendo la furaha.
Je Wewe katika ushirika wako na mwenza wako UNA MAANISHA LIPI KATI YA HAYO?
Kwa sasa wengi wanajikita kwenye HARUSI kuliko kwenye NDOA.
Kwamba unatamani NGUO MAHSUSI KWA TUKIO LA HARUSI na mengine yanayofanana na hayo ili kuufurahisha MOYO wako, Unajua kwamba HARUSI NI TUKIO LA SIKU MOJA ILA NDOA NI KIFUNGO CHA MAISHA?
Magari mazuri yatakayo ipendezesha harusi yako UMEKODI wala hayawezi kuwa sehemu ya FARAJA YA KUDUMU hufikirii baada ya HARUSI ni wewe kuishi kwenye NDOA?
Na hapo ndipo unagundua sababu ya NDOA nyingi kutodumu kwa sababu HARUSI ilitawala akili kuliko NDOA.
Ukiona NDOA imedumu ujue HARUSI haikuwa kipaumbele cha sababu ya wawili hao kukubaliana kujenga UMOJA
Tamaa ya HARUSI imewagharimu wengi, Bila kujua kwamba HARUSI ni sherehe ambayo inakutanisha familia mbili kushiriki FURAHA kwa watoto wao kuamua kuwa WAMOJA.
Kwani baada ya HARUSI mnaobaki kwenye UMOJA WENU ni Mwanaume na Mwanamke wala zile nguo hazitawajenga kwa lolote, Vyakula vikisagwa vinatoweka tumboni KUMBE HARUSI INA LIPI KAMA SIO SHEREHE TU?
Kataa kuwa mtumwa wa MAPICHA PICHA kuwaonyesha watu ulipendeza siku ya HARUSI YAKO maana hayo ni ya kupita ila KIFUNGO ULICHOJIFUNGA NACHO HICHO KITAISHI NAWE DAIMA kumbe hasara ni ya nani?
Fikiria zaidi UMOJA WENU JUU MAISHA YA NDOA kuliko kuwafikiria watu watakavyo ADMIRE Harusi yenu.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria😎
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU