-->

FURAHA SIO KITU CHA AJALI KATIKA MAISHA ILA NI ZAO LA NAMNA UNAVYOISHI NA MWENZA WAKO.

Furaha sio kitu cha ajali katika mahusiano ila ni zao la namna unavyoishi na mwenzako, unachokifanya kwake ndicho kinachoenda kujenga hisia zake na namna anavyokutazama na kukutendea.
Ili akupe furaha ni lazima wewe umpe furaha kwanza kwa sababu kupitia hali yake ya furaha atakupa furaha nawe ili naye aendelee kuwa na furaha. Cha baridi hudumu kwenye baridi kama umoto unavyodumu katika moto, ni kanuni.
Kumbuka hali yako ya kihisia na matendo ni kioo cha tabia ya mwenzako, matendo yako kwake ni kichocheo cha matendo yake kwako.
Chanzo cha yeye kukupa furaha ni wewe kuanza kumpa furaha yeye, kero zako kwake zitazaa kero zake kwako na hatimaye uhusiano wenu kukumbwa na dhoruba.
Kama kiu yako kubwa ni kupata furaha kutoka kwake basi mpe furaha kamili mwenzako kwanza, ukitaka kupokea inabidi kwanza ujifunze kutoa.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU