-->

SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA NA MAFUNZO MENGI


Mwanamke mmoja alitoka nje ya nyumba yake, na akawaona wanaume watatu wazee tena wenye ndevu zao ndefu nyeupe. Wale wanaume walikua wamekaa katika eneo lake kwenye benchi. Yule mwanamke akasema
“…sifikiririi kama nawajua, tafadhali ingieni ndani kuna chochote nitawapa mle”
“Mumeo yupo nyumbani?” waliuliza wale wazee “Hapana, Ametoka” alijibu Yule mwanamke, “Hivyo hatuwezi kuingia ndani kama hayupo” walijibu wale wazee.
Baadae mumewe alivyorudi nyumbani, akamuelezea kilichotokea “Nenda kawambie nipo nyumbani, na uwakaribishe tena ndani” mumewe alisema.
Mwanamke alitoka nje na akawakaribisha wale wazee ndani “Hatuendi ndani wote kwa pamoja” walijibu wale wazee, “Kwanini?” aliuliza Yule mwanamke.
Mmoja wa wale wazee akanza kutoa maelezo: “Jina lake ni UTAJIRI” Alisema huku akimnyoshea kidole rafiki yake, akamuelekezea mwingine kidole akisema “Huyu ni MAFANIKIO, na mimi ni UPENDO” Akaongezea kusema “Sasa rudi ndani na ukajadili na mumeo ni yupi miongoni mwetu mnamtaka nyumbani kwenu”
Mwanamke akarudi ndani na kumwambia mumewe alichoambiwa na wale wazee. Mumewe alijawa na furaha iliyopitiliza “Ni uzuri ulioje” alisema Yule mwanaume “Ngoja tumkaribishe UTAJIRI, ngoja aingie ndani mwetu aijaze nyumba yetu utajiri” Mke wake akakataa “My dear, kwanini tusimkaribishe MAFANIKIO?”
Bint yao mpendwa akaingilia ule mjadala, nae akaja na mapendekze yake “Je isingekuwa bora tukamkaribisha UPENDO? Nyumba yetu sasa itakua imejawa na upendo” “Hebu ngoja tuchukue ushauri wa bint yetu” alisema mwanaume kwa mkewe.
“Toka na umkaribishe Upendo awe mgeni wetu” mwanamke akatoka nje na akawauliza “Ni yupi kati yenu ni Upendo, Tafadhali ingia ndani na uwe mgeni wetu”
Mzee upendo akaamka na kutembea kuelekea katika ile nyumba, wale wenzake nao waliamka pia na kuanza kumfuata mwenzao.
Kwa kushtukiza Yule binti yao akawauliza UTAJIRI na MAFANIKIO “Nimemkaribisha Upendo pekee, kwanini mnaingia ndani?
Wazee wakajibu kwa pamoja “Kama ungemkaribisha UTAJIRI au MAFANIKIO sisi wengine tungebaki nje, Lakini kwa kuwa umemkaribisha UPENDO, Popote aendapo tunaenda nae. Popote kwenye UPENDO, Pia kuna UTAJIRI na MAFANIKIO”
*****_______________________________________*******_____________________*****
NI UKWELI USIOPINGIKA KABISA KWENYE UPENDO LAZIMA UKUWE NA UTAJIRI NA MAFANIKIO. LIKE ZAKO ZIHUSIKE KAMA UMEJIFUNZA KITU. SHARE NA WENGINE.
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU